TAARIFA KWA UMMA
Mkurugenzi Mtenndaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze anapenda kuutarifu Umma kuwa kutakuwa na mkutano wa baraza la Madiwani kwa muda wa siku mbili, siku ya Jumatano ya tarehe 28/08/2019 kutakuwa na mkutano wa baraza la madiwani kwa ajili ya kuwasilisha taarifa za maendeleo ya kata na siku ya Alhamisi ya tarehe 29/08/2019 kutakuwa mkutano wa baraza la madiwani kwa ajili ya taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Mikutano yote kwa siku tajwa hapo juu itaanza saa 4:00 asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri kwa siku zote mbili. Halmashauri ya Chalinze inapenda kuwakaribisha wananchi wote kuhudhuria katika mikutano hiyo.
Imetolewa na
Kitengo cha TEHAMA na UHUSIANO
Halmashauri ya Chalinze
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.