• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Elimu msingi
      • Elimu secondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Maji na umwagiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Vijana
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

JINSI YA KUPATA KIBALI CHA UHAMISHO KWA WATUMISHI WA UMMA

1. Mamlaka za Uhamisho

Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8. ya mwaka 2002 ikisomwa na Kanuni zake pamoja na Taratibu za Uendeshaji za mwaka 2003   Mamlaka ya Uhamisho kwa watumishi wote wa Umma ni Katibu Mkuu  Ofisi Ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma na

Kwa  maelekezo ya Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi Wa Umma kwa barua Kumb Na. C/CB.271/431/01/62 ya tarehe 8/06/2006 na Kumb Na. C/CB.271/431/01/J/144 ya tarehe 27/08/2007 Mamlaka ya Uhamisho katika Uhamisho wa  watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa  yamekasimiwa kwa;

  1. Katibu Mkuu Ofisi Ya Waziri Mkuu TAMISEMI kwa watumishi wanaohama kutoka  Halmashauri moja kwenda nyingine nje ya Mkoa;
  2. Katibu Tawala Mkoa  kwa   uhamisho wa watumshi wanaotoka Halmashauri moja kwenda nyingine ndani ya Mkoa na; 
  3. Mkurugenzi wa Halmashauri kwa watumishi wanatoka kituo kimoja   kwenda  kingine ndani ya Halmashauri.

2. Aina za Uhamisho

Kuna aina mbili za Uhamisho, nazo ni;

  1. Uhamisho wa Kuomba
    1. Taratibu za Kuomba Nafasi:-

    2. Mtumishi atapaswa kuomba nafasi ya uhamisho kwa kuwasilisha maombi yake ya uhamisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri au Mamlaka anayotaka kuhamia kupitia kwa Wasimamizi wake wa kazi katika kituo chake cha kazi alichopo na Mkurugenzi wake.
    3. Wasimamizi wa mtumishi anayeomba uhamisho  watapaswa kuhakikisha maombi ya mtumishi yanafika katika mamlaka husika yakiwa na maoni yao kuhusu maombi hayo na sio kuzuia maombi. Iwapo kutakuwa na sababu ya msingi ya kuzuia maombi mwajiri amjulishe mtumishi kwa kumrejesha katika miongozo iliyopo 
    4. Iwapo Mwombaji hataridhika na maoni /sababu za mwajiri /Msimamizi wa kazi kukataa maombi yake  mwombaji atawasilisha maombi yake kwa  Katibu  Tawala wa Mkoa kwa ushauri na kama hataridhia maombi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI  yakiwa na vielelezo muhimu kuthibitisha maombi hayo kukataliwa na Mkurugenzi na kueleza sababu za  yeye kuomba uhamisho huo.
    5. Mkurugenzi/Msimamizi wa kazi  atayeombwa nafasi ya kuhamia atapaswa kumjibu mtumishi kupitia kwa Mkurugenzi wake  kwa barua akimweleza kupatikana kwa  nafasi hiyo  kumetokana na nini ikiwa ni pamoja na kutaja  Check Namba za watumshi waliofariki au kuacha kazi. 
    6. Iwapo mtumishi wa umma ataomba uhamisho kwa sababu za kumfuata mume au mke, kujiandaa kustaafu baada ya kukaa miaka kumi nje ya mkoa anaotarajia kustaafia na kukaa katika kituo kimoja kwa zaidi ya miaka mitano anaweza kufikiriwa kugharamiwa gharama za uhamisho hata kama ataomba uhamisho mwenyewe.
    7. Mtumishi anayeomba uhamisho atapaswa kuwasilisha maombi yake kwa Katibu Mkuu au Katibu Tawala Mkoa au Mkurugenzi  akiambatanisha barua iliyomkubalia kuhamia katika kituo anachotaka kuhamia.  Aidha ni muhimu amjulishe mwombaji iwapo  atagharimiwa uhamisho au la kufuatia kupata nafasi hiyo
    8. Upatikanaji wa Majibu:-

      Hairuhusiwi Mtumishi yeyote kutumia mtu mwingine isipokuwa yeye mwenyewe au Mwajiri wake kwa njia ya posta au Mkono kuwasilisha maombi yake ya uhamisho. Inashauriwa kutumia njia ya EMS au regista kwa urahisi wa ufuatiliaji.

      Angalizo:

    9. Watumshi wote walioomba uhamisho watapata majibu yao kwa barua kupitia kwa waajiri wao na sio vinginevyo.
    10. Aidha kwakuwa uhamisho huu ni wa wazi watumishi waliokubaliwa au kaukataliwa uhamisho watapata taarifa za awali  kupitia Tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI yaani www.pmoral.go.tz mapema mwezi Julai  kwa maombi yatakayopokelewa kuanzia Januari  hadi Juni na mapema mwezi Januari kwa maombi yatayopokelewa kuanzia mwezi Julai hadi Desemba kwa kuwa Ofisi yetu imejipanga kushughulikia masuala ya uhamisho mara mbili kwa mwaka  ili kuepusha mwingiliano wa majukumu  katika vituo vya kazi kwa mwaka. 
    11. Mtumishi atakayekuwa na malalamiko kuhusu maombi yake ya uhamisho anashauriwa kuelekeza maombi yake kwa Mamlaka iliyomwamisha kupitia kwa mwajiri wake na msimamizi wa kazi akiambatisha maombi yake ya awali na vilelezo vingine muhimu kama sababu za kuomba uhamisho na ushahidi wa kufikisha barua yake kwa Mamlaka ya uhamisho.
    12. Malalamiko ya mtumishi aliyeomba uhamisho na hakupata majibu au hakuridhika na majibu aliyopatiwa malalamiko yake yatashughulikiwa ndani ya siku saba bila kujali muda wa uhamisho yaani June au Desemba. 
    13. Baada ya mtumshi kupata majibu /barua ya uhamisho atapaswa kuripoti ndani ya siku kumi na nne tangu amekabidhiwa barua yake ya uhamisho vinginevyo atachulikuliwa ni mtoro kazini.
  2. Uhamisho wa Kawaida

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2018 January 24, 2019
  • TANGAZO LA MKUTANO WA BALAZA LA MADIWANI ROBO YA NNE August 28, 2019
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA PWANI December 18, 2018
  • TANGAZO LA KUSITISHWA KWA UHAMISHO August 31, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mafunzo ya Kuwajengea Uwezo Madiwani Yatolewa Chalinze

    December 21, 2020
  • Kamati ya Ushauri ya Wilaya ya Bagamoyo Yaridhia Chalinze kuwa Wilaya.

    December 19, 2020
  • Madiwani waridhia Kuanzishwa Wilaya Mpya ya Chalinze

    December 18, 2020
  • Baraza la Madiwani Chalinze Limezinduliwa

    December 18, 2020
  • Tazama zote

Video

Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akihimiza ukusanyaji Mapato kwenye mamlaka za serikali za Mitaa
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • Mfumo wa Bajeti
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2015/2016
  • WAZO LA WAZIRI
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • JINSI YA KUJISAJILI NA KUPATA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN NAMBA)

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Lugoba Chalinze

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.