Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze jana wameanza rasmi mafunzo ya kujengewa uwezo Baada ya kuwa wamekula kiapo cha Utii, mafunzo hayo yatafanyika kwa siku nne mfululizo.
Mafunzo hayo yametolewa na Wataalamu kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo. Wataalamu hao wameweza kuwajengea uwezo Madiwani katika mada mbalimbali za namna ya uendeshaji wa serikali Mitaa Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Madiwani wamewezeshwa katika Uongozi na Utawala Bora,Historia na Uhalali wa Serikali za Mitaa, Sheria za Uendeshaji wa Serikali za Mitaa, Kanuni Kuhusu Maadili ya Madiwani, Usimamizi wa Watumishi katika Serikali za Mitaa,Uibuaji,Upangaji na Usimamizi wa Mradi Shirikishi Katika Jamii, Usimamizi na Udhibiti wa Fedha Katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, Taratibu za Mikutano na Uendeshaji wa Serikali za Mitaa na Wajibu, Majukumu,Haki na Stahiki za Madiwani.
Aidha Katika mafunzo hayo Madiwani walifurahia mafunzo hayo na kuahidi kuyatumia maarifa waliyoyapata kwa maslahi ya wanachalinze na watanzania kwa ujumla.Waliomba mafunzo ya namna hii yawe endelevu ili kuwawezesha kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni,
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Geofrey Kamugisha kwa niaba ya Madiwani wenzake aliwashukuru wataalamu kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kwa kuwajengea uwezo kupitia mada walizowasilisha."Kupitia mafunzo haya tumepata ufahamu wa kutosha juu ya Historia na Uhalali wa Serikali za Mitaa na namna ya Uendeshaji wa Serikali za Mitaa,"Kamugisha alisema.
Naye Diwani wa kata ya Msoga Mheshimiwa Hassan Mwinyikondo aliishukuru Halmashauri kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yamewapa mwanga kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Mamlaka za Serikali za Mitaa na kushauri ni vema Mafunzo haya yawe yanatolewa kwa pamoja yaani wataalamu na waheshimiwa Madiwani ili kujadili masuala mbalimbali na kuondoa misuguano katika utekelezaji wa majukumu.
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.