Maafisa Bajeti wa Halmashauri ya Chalinze,kwa maana ya waandaaji wa bajeti kutoka Idara na Vitengo mbalimbali ndani ya Halmashauri wamepata mafunzo juu ya matumizi sahihi ya mfumo wa mpango na bajeti (Planrep) kwa ajili ya maandalizi ya bajeti.
Mafunzo hayo yametolewa leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Chalinze na wataalamu wa Idara ya Mipango ili kurahisisha maandalizi ya mpango bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022,ambayo yanaendelea.
Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili mfululizo na baada ya hapo kazi ya uandaaji wa bajeti itaendelea kwa kila Idara na hatimaye kupata bajeti ya Halmashauri nzima.
Akizungumza na Ofisi ya Habari Mkuu wa Idara ya Mipango Bwana Shabani Millao amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa maafisa wanaotumia mfumoo katika maandalizi ya bajeti,kwani mfumo huu umefanyiwa marekebisho tofauti na Mfumo wa mwaka uliopita. Hivyo amewataka washiriki kuwa makini katika Mafunzo hayo ili kuweza kufanya kazi zao bila kikwazo.
Lugoba Chalinze
Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze
Simu: +255232935403
Simu ya mkononi:
Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz
Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.