• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Serikali kuendeleza utatuzi na uimarishaji wa miundombinu ya mawasilino Chalinze na nchi nzima.

Imewekwa: March 1st, 2021

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari - Mhe. Mhandisi. Andrea Mathew Kundo leo Tarehe 01.03.2021 amefanya ziara Halmashauri ya Chalinze ili kujionea utekelezaji wa mambo mbalimbali yanayohusu Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) yanayofanya na Halmashauri ikiwemo kutatua Changamoto zinazoikumba Halmashauri ya Chalinze hususani katika maswala ya  Mawasiliano.

Akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Halmashauri katika maswala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Ndugu. Ramadhani Possi alieleza zipo changamoto nyingi za mawasiliano ikiwemo kutokupatikana kwa mitandao ya simu katika baadhi ya maeneo jambo ambalo huleta changamoto hata katika ukusanyajiwa mapato kwani mashine za kielektroniki zinazotumika katika utoaji wa risiti huhitaji mtandao ili zifanye kazi. Aidha Ndugu Possi aliongezea kuwa Halmashauri ya Chalinze ipo katika mchakato wa kuanziasha Radio ya Umma na imekwisha tuma barua TCRA kwa ajili ya kupata masafa (Frequency) pasipo mafanikio ya kupata masafa hayo.

Nae, Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete alimueleza Naibu Waziri kuwa uimara wa mawasiliano ni pamoja na kupata vyombo vya mawasiliano kama Redio na Televisheni ili kuwezesha upashanaji wa habari ya mazuri yanayofanyika katika Wilaya yetu na Tanzania kwa jumla.

"Mhe. Naibu Waziri leo umekuja hapa Jimboni utatupatia mwanga mpya kupitia mawasiliano yetu. Jimbo letu limekuwa na shida katika mawasiliano kwa muda mrefu matatizo ambayo yana sura zinazofanana katika utatu wake” Alisema Mh Ridhiwani.

 Akieleza juu ya shida hiyo Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Kikwete alitoa mfano wa kijiji cha Matipwili na Kijiji cha Mkoko jinsi wanavyopata shida katika mawasiliano ya Simu, Mheshimiwa Mbunge alieleza shida kubwa ya vijiji vyote zinafanana ambapo mitambo hiyo hupatikana baadhi ya maeneo na maeneo mengine kukosekana, pia matatizo mengine yakiwemo yale ya mawasiliano kukosekana barabarani kati ya kijiji na kijiji au miji na miji na kutolea mfano kijiji cha Kwa Mduma na Kitongoji cha Gole hivyo endapo mtu atapata shida njiani inakua ngumu sana kupata msaada wa haraka.

Akijibu juu ya Changamoto alizo elezea Mbunge Naibu Waziri Teknolojia, Habari na Mawasiliano Mhe. Mhandisi. Andrea Mathew Kundo alimuhakikishia Mbunge na wananchi wa Chalinze kuwa serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa matatizo ya mawasiloiano yanapungua kama sio kumalizika abisa, pia ili kutosababisha hasara kwa makampuni ya simu serikali inaangalia thamani ya biashara iliopo katika maeneo husika kwa kupitia Mfuko wa mawasiliano kwa Umma ili kuwapatia wannchi hudama zilizo bora na za uhakika pasipo kuathiri mitaji wa wawekezaji.

Mh. Mhandisi Kundo amebainisha kuwa, kukosekana kwa radio Halmashauri inasababisha Wananchi kushindwa kusikia mambo mazuri yanayofanywa na Serikali yao chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

"Wananchi wanataka kusikia mambo yanayofanywa kwenye Halmashauri yao. Pia wanataka kusikia Diwani wao kafanya nini au Mbunge wao kafanya jambo gani ili kupunguza maswali wakati wa kazi au kwenye mikutano ya viongozi wao ama kwa Serikali yao". Alisema Mhandisi Kundo.

"Mh. Ridhiwani Kikwete aliniuliza juu ya tulipofikia suala la masafa ya Radio. Kiukweli suala ili nimelijua jana na leo nimefika hapa hivyo basi ninamwagiza Mkuu wa Kanda wa Mashariki wa TCRA ambaye yupo hapa ahakikishe analifanyia kazi na hadi jioni ya leo niwe nimepata majibu ya kurejesha kwa Mbunge’ alisema Mhandisi Kundo.

Akijibu changamoto za Upatikanaji wa Masafa ya Radio Mh. Mhandisi Kundo amemwagiza Meneja wa Kanda wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kanda ya Mashariki kushughulikia haraka maombi ya Halmashauri ya Chalinze ya kuimarisha miundombinu ya mawasiliano ikiwemo kupatiwa kibali cha  Masafa ya radio (radio frequency) ambayo yalikwama kwa muda mrefu.

Aidha, akijibu suala la changamoto ya upatikanaji wa mawasiliano baadhi ya maeneo ya Jimbo la Chalinze, Naibu Waziri alibainisha kuwa, kumekuwa  na changamoto ya usimikwaji wa minara mipya ya Mawasiliano  katika baadhi ya maeno inanayosababishwa na upatikanaji wa vibali.

"Vibali vimekuwa vikichukua muda mrefu kuanzia miezi mitatu hadi tisa kwani hupita kwenye mamlaka nyingi kabla ya kibali hicho kutoka, lazima upate kibali cha eneo, upate kibali kutoka mamlaka ya Anga na kuna wenzetu wa Mazingira (NEMC) ambao wao kibali chao huchukua hadi miezi Sita ndipo upewe kibali cha ujenzi. Lakini nina hakika masuala haya yatafanyiwa kazi na mawasiliano yatakuwa vizuri, Hata hivyo Serikali kupita mfuko wa mawasiliano kwa wote (ambao ulianzishwa kwa lengo la kupeleka mawasiliano katika maeneo ambayo hayana mvuto wa kibiashara) imeanza kutoa ruzuku ya ujenzi wa minara ya simu na hadi sasa jumla ya kata 1057 zimekwisha jengewa minara na katika Halmashauri ya Chalinze TTCL walishinda kandarasi ya Ujenzi wa minara Kata ya Mkange katika vijiji vya Mandamazingara, Matipwili na Mkange kijijini tarehe 24/01/2021 na wanategemea kukamilisha ujenzi huo mwezi wa tisa mwaka huu kwani kwa sasa wapo katika hatua ya manunuzi ya vifaa" alisema Mh. Mhandisi Kundo.

Akihitimisha ziara yake katika kata ya msata amewataka wanchi wa Chalinze na Taifa kwa ujumla kuwa wavumilivu wakati serikali yao sikivu ikiendelea na utatuzi wa changamoto ya Mtandao ambazo zinaikumba nchi hii, kwani Serikari ipo katika zoezi la usabazaji wa Mkongo wa taifa ambapo mpaka sasa jumla ya Kilometa 7,910 zimekwisha fikiwa kati 86,000 zinazohitajika kwa nchi nzima ikiwa ni lengo la Serikali kufikisha katika Mikoa, Wilaya na Kata na siku za mbeleni kufikisha katika familia. Aidha amewataka viongozi wa malaka zote ambazo amewapa maagizo kuyafanyia kazi maagizo yote tena kwa wakati ili wananchi waweze kupata huduma ya mawasiliano kwa urahisi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.