• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Shule Kumi Bora zatunukiwa Vyeti Chalinze

Imewekwa: March 3rd, 2020


Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze mkoani Pwani leo imezitunuku vyeti shule zipatazo 20 zilizofanya vizuri katika matokeo ya darasa la Saba na la nne kitaifa kwa mwaka 2019, na kuwa miongoni mwa shule kumi bora kwa ufaulu.


Hafla ya kutoa tunu hizo imefanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze na kushuhudiwa na Madiwani wa halmashauri hiyo, kabla ya kuanza kwa mkutano wa Baraza la Madiwani unaoendelea leo katika halmashauri ya Chalinze.


Mgeni rasmi katika hafla ya kutoa tunu hizo alikuwa ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Mheshimiwa Saidi Zikatimu. Zikatimu amewatunuku Walimu wakuu wa shule hizo kama ishara ya ufanisi wa shule hizo.


Kwa mujibu wa Afisa Elimu Msingi Bi Zainabu Juma Makwinya alizitaja shule zilizofanya vizuri katika mitihani hiyo kwa kuanza darasa la nne kuwa ni; Chalinze Modern Islamic Seminary,Berachah Valley,Magome,St. Alphonso,Pakistani Mtete,Mustlead,Pingo,Bomani na Sirajul Munir Kiwangwa.


Kwa upande wa darasa la Saba,shule kumi bora zilizotunukiwa vyeti ni Chalinze Modern Islamic,Honest, Sirajul Munir Kiwangwa,Ndossam,Kibiki,Mdaula "B",Tukamisasa,Matuli,Ubenazomozi na Saadani Chumvi.


Mgeni rasmi katika hotuba yake ya kutunuku vyeti alizipongeza shule zote zilizoibuka kidedea na kuwapongeza Walimu na wanafunzi kwa kutekeleza wajibu wao katika suala zima la kitaaluma na kuzitaka shule zingine ziongeze bidii katika suala zima la Elimu na kuinua ufaulu ili taifa liweze kupata wataalamu mbalimbali wa kulitumikia Taifa.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bi Amina Kiwanuka ametaka uwepo ushirikiano kati ya wazazi,walimu na wanafunzi katika suala zima la kujifunza ili tuwe na matokeo yenye tija katika halmashauri yetu na hatimaye Halmashauri kuwa katika nafasi bora kimkoa na kitaifa.


Aidha hafla ya kuzipongeza shule bora katika halmashauri zilishuhudiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete, pamoja na wananchi waliokaribishwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani.


Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete aliwapongeza walimu wote jimboni Chalinze kwa kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuwawezesha wanafunzi kufaulu kwa kiwango hicho na kutoa wito kwa walimu wote jimboni Chalinze kuwa na moyo wa kizalendo katika kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano kwa kutoa Elimu pasipo malipo.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.