• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Rasilimali watu na utawala
      • Elimu msingi
      • Elimu secondari
      • Mifugo na Uvuvi
      • Usafi na Mazingira
      • Maji na umwagiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na ufuatiliaji
      • Afya
      • Ardhi na maliasili
      • Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Vijana
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Tehama na Uhusiano
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Waziri Mhagama akerwa na ucheleweshwaji wa ujenzi wa Zahanati ya Mdaula Maabara na Kituo cha ushauri nasaha Chalinze

Imewekwa: February 27th, 2021

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu (Sera, Bunge na watu wenye ulemavu) Mh. Jenista Joackim Mhagama leo tarehe 27.02.2021 amefanya ziara na kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa Halmashauri ya Chalinze kwa fedha zilizotolewa na Benki ya dunia na kusimaniwa na TACAIDS na TANROAD ili kusaidia mapambano dhidi ya UKIMWI  kwa watu wanaoishi eneo la mradi na wale wanaopita katika eneo hilo kama wasafiri na madeleva wanaopumzika katika maeneo ya chalinze kabla yakuendelea na safari zao.

 Akiwa ziarani Chalinze Mh. Mhagama alibaini ucheleweshwaji wa ukamilishaji wa Miradi hiyo inaotekelezwa Katika Kituo Cha afya Chalinze na Mdaula licha ya fedha za utekelezaji kuwa zimekwisha lipwa tangu mwezi wa kwanza mwaka huu

Sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hii ukizingatia fedha kwa ajili ya ukamilisha wa kazi mliopewa imekwisha lipwa tangu Januari mwaka huu. Alisema Mh. Mhagama

Aidha alimtaka mkandarasi alieingia mkataba wa kutekeleza ujenzi wa Zahanati ya Mdaula, Maabara na Jengo la ushauri nasaha kwa watu wenye maambukizi katika Kituo cha afya Chalinze na Mdaula kuhakikisha anakamilisha ndani ya miezi miwili na yeye mwenyewe atakuja kulifungua mwisho wa mwezi wa nne.

'Ninawaagiza miradi yote mliopewa kutekeleza hakikisheni inakamilika kabla ya tarehe 25.04.2021 na  nitatuma maafisa toka ofisi yangu kuja kukagua na tarehe 30.04.2021 nitakuja kuzidua huduma katika majengo haya pale nitakapo jiridhisha kuwa yamekamilika kwa viwango vinavyohitajika'  Alisema Mh. Mhagama

Lengo la serikali yetu ya awamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wetu Msikivu Mh. Dr John Pombe Magufuli ni kuhakikisha huduma zinazohusu mapambano dhidi ya UKIMWI zinapatikana kila eneo kwa lengo la Kutoa elimu ya mapambano dhidi ya UKIMWI,Upimaji na Utoaji dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI zinapatikana kila sehemu, Aliongeza Waziri Muhagama.

Akitoa takwimu za maambuki ya UKIMWI kutokana na tafiti zilizofanyika mwaka 2019. Mh Mhaghama alisema "jumla ya maambukizi duniani ni  takribani watu milioni 38  na kati ya walioathirika hao wengi wanaotoka nchi za Afrika na nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ambao wanafikia jumla ya waathirika milioni 20.7 ambapo Tanzania maambukizi ni milioni 1.7, hivyo kutokani na uboreshaji wa miundo mbinu uliofanywa na Serikari ya awamu ya tano imesababisha Tanzania kufunguka kibiashara na kimahusiano na Nchi zingine tunahitaji kujipanga ili kuzuia maambukizi mapya. Jambo hili lilipelekea Serikali kutenga bajeti na kwa kutumia wahisani kujenga vituo hivi 20 Nchi nzima kutoka Dar es Salaam hadi maeneo ya mipakani ili kuzidisha mapambano haya dhidi ya UKIMWI . Zaidi ya Fedha za kitanzania Milioni 600 zimeletwa  Chalinze ili kukamilisha ujenzi wa Jengo la ushauri na nasaha na Maabara kituo cha Afya Chalinze na Zahanati ya Mdaula.

Nae Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani J Kikwete katika ziara hiyo alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dr John Joseph Pombe Magufuri kwa kuendelea kuijali Chalinze kwani nje ya zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 600 ambazo ametoa kwa ajili ya miradi aliokuja kuikagua Mh.Mhagama takribani Fedha za kitanzania Bilioni Moja zimeletwa kwa ajili ya Ujenzi wa jengo la huduma ya mama na mtoto, maabara, wodi maalumu ya kinababa na kumalizi uimarishaji wa miundombinu ya Duka la dawa Hospitari ya Wilaya Chalinze iliopo kata ya Msoga ili kunusuru maisha ya wajawazito akina mama waliojifungua na watoto alimpongeza Mh. Mhagama kwa kuteuliwa kuwa waziri na kutaka aendeleze kasi aliokujanayo katika kusimamia wizara hiyo ili mambo yote ambayo yamekua yakikwama yaweze kufanikiwa kwa mustakabari wa Wanachalinze na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza juu ya miradi iliotembelèwa Mh Ridhiwani alisema " Nina laani vikari juu ya ucheleweshwaji wa miradi hii ulioitembelea leo kwa kua hapakuwa na sababu kwani Kampuni lililopewa mkataba wa ujenzi (Kihure Company Ltd) nilimekwisha lipwa fedha za mradi.

Nakushukuru kwa maagizo yako kuwa ndani ya miezi miwili miradi yote miwili iwe imekamilika nami kama kiongozi wa eneo hili nakuahidi kufuatilia kwa karibu maendeleo ya ujenzi huo kwa kushirikiana na viongozi wenzangu akiwemo Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri Jeofrey Kamugisha Diwani wa Bwilingu Mh. Nassa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri Ndugu. Ramadhani Possi, aliongeza Mh. Ridhiwani

Mh. Mhagama Alihitimisha ziara yake kwa kuongea na wananchi waliokuwa wamekusanyika ili kutoa kero zao ikiwemo kuchelewa kwa kumalizika kwa zahanati ya Mdaula. Aidha Mh. Mhagama aliwataka TANRIAD, TACAIDS na uongozi wa Jimbo la Chalinze akiwemo Mh. Ridhiwani (Mbunge), Jeofrey Kamugisha (M/Kiti) Mh. Nassa (Diwani kata ya Bwilingu) na Ndugu Ramadhani Possi (Mkurugenzi) kukaa meza moja ya majadiliano ili kujua ukomo wa utekelezaji wa mradi kwa fedha zilizotolewa na Serikalo ili kutumia fedha za mapato ya ndani kiasi cha Milioni 10 kukamirisha sehemu ya mradi itakayobaki ikiwemo kununua samani na vifaa tiba baada ya kupewa taarifa kuwa havimo katika mkataba wa mkandarasi anaetekeleza wa mradi huo

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE CSEE 2018 January 24, 2019
  • TANGAZO LA MKUTANO WA BALAZA LA MADIWANI ROBO YA NNE August 28, 2019
  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MKOA WA PWANI December 18, 2018
  • TANGAZO LA KUSITISHWA KWA UHAMISHO August 31, 2018
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Soko la kisasa Halmashauri ya Chalinze kuamilika Juni 2021

    April 09, 2021
  • Halmashauri ya Wilaya Chalinze yafanya Dua kumuombea Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

    April 07, 2021
  • Watendaji simamieni majukumu yenu na kufanya maamuzi kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu

    March 16, 2021
  • Kilio cha wananchi wa Kaloleni Chaigusa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa

    March 13, 2021
  • Tazama zote

Video

Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akihimiza ukusanyaji Mapato kwenye mamlaka za serikali za Mitaa
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • Mfumo wa Bajeti
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2015/2016
  • WAZO LA WAZIRI
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • JINSI YA KUJISAJILI NA KUPATA NAMBA YA MLIPA KODI (TIN NAMBA)

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Lugoba Chalinze

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.