• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Chalinze Afungua mafunzo ya waandikishaji

Imewekwa: May 15th, 2025

AFISA MWANDIKISHAJI WA JIMBO LA CHALINZE AFUNGUA MAFUNZO YA WAANDIKISHAJI


Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, leo amefungua rasmi mafunzo ya watendaji wa kata kuhusu zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete na yamelenga kuwaandaa watendaji hao kwa kazi ya uandikishaji itakayodumu kwa siku saba mfululizo kuanzia Ijumaa, tarehe 16 Mei hadi 22 Mei 2025.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Bwana Possi amewataka waandikishaji kufanya kazi hiyo kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi. Amesisitiza kuwa uandikishaji ni kazi nyeti inayohitaji uadilifu, uwajibikaji na ufuatiliaji wa maelekezo yote yanayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


Bwana Possi amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hili muhimu, hususan wale ambao hawakupata nafasi ya kujiandikisha katika awamu zilizopita. Amesema huu ni wakati wa kila Mtanzania kutumia haki yake ya kikatiba kwa kuhakikisha amejiandikisha ili aweze kushiriki uchaguzi wa viongozi anaowataka.


Aidha, Afisa Mwandikishaji huyo ametoa wito kwa wananchi waliojiandikisha tayari kufika katika vituo vyao kuhakiki taarifa zao, na pale zitakapokuwa na makosa, wafanye marekebisho ili taarifa zao ziwe sahihi kwenye daftari.


Kabla ya kuanza mafunzo yao, waandikishaji wote wa ngazi ya kata walikula kiapo cha utii pamoja na kiapo cha kujiondoa katika uanachama wa vyama vya siasa, kama inavyoelekezwa na sheria na maadili ya uchaguzi, ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa weledi na bila upendeleo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.