• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Bilioni 50.6 kuidhinishwa na Baraza la Madiwani Chalinze

Imewekwa: February 19th, 2019

Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze limekaa na kupitisha bajeti ya Mapato na matumizi ya jumla ya Fedha za kitanzania bilioni 50.6 kwa mwaka wa Fedha 2019/2020.Mapendekezo ya bajeti hiyo yamefanyika katika kikao maalumu cha baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa shule ya Sekondari ya Lugoba jana.

Akiwasilisha bajeti hiyo Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bwana Shabani Millao alitoa ufafanuzi wa bajeti na kueleza mawanda ya bajeti(scopes of budget)hiyo kuwa,Mapato ya ndani bilioni 6.1,michango ya Jamii bilioni 1.8,ada za shule za Sekondari milioni 84.6,mishahara bilioni 31.7,miradi ya maendeleo serikali  kuu bilioni 5.8,ruzuku ya matumizi ya kawaida bilioni 3.9,wahisani bilioni 1.2. Hivyo kutokana na ufafanuzi huo bajeti ya halmashauri ya Wilaya ya Chalinze inakuwa na bajeti yenye  jumla ya Fedha za kitanzania  bilioni 50.6.

Katika mapendekezo ya bajeti baraza la Madiwani lilipitia kwa kina kamati kwa kamati na kuona vipaumbele ambavyo vinatatua kero za wananchi kama huduma za afya,elimu Maji na usafi wa mazingira na wajumbe walishauri baadhi miradi iondolewe kwa sasa ili huduma za Jamii zitolewe moja kwa moja,katika mabadiliko ya miradi waliyopendekeza wajumbe ni kuondoa mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara na kukamilisha vituo vya afya ,zahanati na vyumba vya madarasa ambavyo ni kipaumbele kwa sasa.Naye Diwani wa viti maalum CCM Maria Moreto aliwaomba Madiwani kumuunga mkono hoja ya kuondoa mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara kwa sasa ili kukamilisha miradi ya wananchi na wananchi waanze kupata huduma, mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa idara ufanyike bajeti ijayo.   Mwenyekiti Wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe Saidi Zikatimu alitoa mchango wake wa mawazo kwa kueleza umuhimu wa miradi katika halmashauri na kuwataka wajumbe kuamua kwa kuzingatia miongozo ya bajeti na si vinginevyo kwani tunapanga bajeti kwa miongozo iliyotolewa na serikali.    Kwa upande wake Diwani wa kata ya Miono ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mheshimwa Juma Mpwimbwi aliwapongeza wataalamu kwa maandalizi mazuri ya bajeti na kwa ufafanuzi mzuri wa mawanda ya bajeti Iliyofafanuliwa na Kaimu Mkurugenzi, "Ni bajeti inayogusa Maisha ya wananchi na inayotatua kero za wananchi katika halmashauri yetu,bajeti hii itatekelezeka kama tutakusanya Mapato yetu kwa umakini na kufikia malengo tuliyojiwekea." Mpwimbwi alisema.    Naye Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bwana Shabani Millao aliwashukuru wajumbe wa baraza la Madiwani kwa kupitia kwa kina bajeti pendekezwa na kueleza kuwa bajeti hii imeandaliwa kwa kuzingatia miongozo ya serikali na kila kinachosomeka ni kipaumbele kwani mwongozo ndiyo uliotumika katika kuandaa kazi hii. "Ushauri mlioutoa ni wa kujenga na pale itakapowezekana kulingana na ukomo wa bajeti tutatekeleza na ikishindikana kwa mwaka huu tutatekeleza kwa bajeti ijayo“ Millao alisema.     Hata hivyo baada ya mjadala wa muda mrefu kwa pamoja Madiwani waliridhia kupitisha bajeti ya halmashauri yenye thamani ya Fedha za kitanzania bilioni 50.6.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.