• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Baraza la Ushauri wilaya ya Bagamoyo (DCC) lapokea taarifa ya Utekelezaji 2021/2022

Imewekwa: November 28th, 2022


Baraza la Ushauri la wilaya ya Bagamoyo(DCC) limepokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Taarifa hiyo imewasilishwa na Afisa Mipango wa Halmashauri ya Chalinze Bwana Shabani Millao kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze.


Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa kujumuisha Halmashauri zote mbili za Bagamoyo na Chalinze na Taasisi zinazofanya kazi katika Halmashauri hizo kwa maana ya TARURA,RUWASA,TRA,TANESCO na DAWASA. Taasisi zote hizo zimewasilisha taarifa za utekelezaji wa Majukumu mbalimbali kwa mujibu wa mipango kazi ya Taasisi hizo na kujadiliwa na wajumbe wa kikao hicho kwa kuzingatia ufanisi na changamoto zinazoyakabili mashirika hayo.


Katika kikao hicho kinachofanyika kila mwaka mara mbili kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake ni kikao kinachofanyika kwa misingi ya kupokea taarifa za utekelezaji na kutoa ushauri kwa utendaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Zainab Abdallah akiongoza Kikao hicho baada ya taarifa za utekelezaji kwa kila Halmashauri, Mkuu wa wilaya alizitaka Halmashauri kuwa na miradi ya kimkakati ambayo itaziwezesha Halmashauri kuzalisha fedha kutokana na uwekezaji unaotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri.


Kwa upande wa Taasisi za umma zinazojitegemea alizitaka kutoa huduma kwa wananchi kwa weledi kwa kuhakikisha miundombinu ya barabara,Maji na Umeme inawafikia wananchi pasipo shaka na Kuhakikisha wanatatua kero kwa muda mara zinapojitokeza bila kuchelewa.


“Halmashauri ni wataalam na Madiwani niwatake mfanye kazi kama timu ili kuwaletea Maendeleo wananchi na kila mmoja asimame kwenye nafasi yake kwa kutekeleza majukumu yake,tubadilike ndugu zangu.” Mkuu wa wilaya alisema.”


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze,Mheshimiwa Hassani Mwinyikondo aliwataka washiriki wa kikao hicho kwa maana ya wataalam wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mashirika yanayojitegemea kuwa na moyo wa kizalendo katika kuwatumikia wanachalinze na watanzania kwa ujumla ili kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kama kilivyowaahidi watanzania.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Bwana Ramadhani Possi akichangia katika baraza hilo aliahidi kuyafanyia kazi maoni mbalimbali yaliyotolewa na wajumbe kwa misingi ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi sanjari na kuibua miradi ya kimkakati ambayo itakuwa na tija kwa Halmashauri na kuwa endelevu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.