• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Baraza la wafanyakazi Chalinze lapitisha mapendekezo ya bajeti 2026/27

Imewekwa: February 10th, 2026

Baraza la Wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze limepitisha mapendekezo ya bajeti ya stahiki za watumishi kwa mwaka wa fedha 2026/27, ambapo jumla ya shilingi bilioni 4.25 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia stahiki mbalimbali za watumishi wa Halmashauri hiyo.


Bajeti hiyo, iliyowasilishwa mbele ya Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la Wafanyakazi, inalenga kuboresha ustawi wa watumishi kwa kugharamia stahiki ikiwemo likizo, matibabu, uhamisho, mazishi, mafunzo, sare za kazi, posho za kujikimu, masaa ya ziada, pamoja na gharama za pango, umeme na simu kwa Wakuu wa Idara na Vitengo.


Kwa mujibu wa makisio hayo, Halmashauri imetenga shilingi milioni 369 kwa ajili ya likizo, shilingi milioni 266.5 kwa uhamisho, shilingi milioni 18 kwa matibabu na shilingi milioni 83.3 kwa ajili ya mazishi ya watumishi. Aidha, shilingi milioni 228.69 zimetengwa kwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu, huku shilingi milioni 25 zikitengwa kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wafanyakazi 50 watakaobainika kuwa hodari katika utendaji kazi.


Katika hatua nyingine, Baraza limepokea taarifa ya upandishwaji vyeo kwa jumla ya watumishi 1,293 wanaotarajiwa kupandishwa vyeo kutokana na utendaji mzuri na muda wa utumishi wao. Pia, shilingi milioni 186 zimetengwa kwa stahiki za Wakuu wa Idara na Vitengo, na shilingi milioni 46.85 kwa ajili ya sare za kazi kwa watumishi wa idara na vitengo mbalimbali.


Kuhusu ajira mpya, imeelezwa kuwa katika mwaka wa fedha 2026/27 Halmashauri imetenga nafasi 120 za ajira katika sekta za elimu, afya na ujenzi, huku Baraza likitoa pongezi kwa Serikali kwa kuipatia Halmashauri jumla ya watumishi wapya 123 katika kada mbalimbali, hususan afya, elimu sekondari, kilimo na mifugo pamoja na maliasili na mazingira.


Sehemu kubwa ya bajeti imetengwa kugharamia posho za kujikimu na masaa ya ziada, ambapo shilingi bilioni 1.25 zimetengwa kwa posho za kujikimu na shilingi bilioni 1.35 kwa ajili ya posho za masaa ya ziada kwa watumishi wa idara mbalimbali, fedha zitakazotokana na mapato ya ndani pamoja na ruzuku kutoka Serikali Kuu.


Baraza la Wafanyakazi pia limejadili mikakati ya utekelezaji wa bajeti hiyo ikiwemo kuhakikisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa asilimia 100, kuendelea kupata ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kulipa stahiki za watumishi, pamoja na kuimarisha usimamizi na uwajibikaji kwa watumishi wote.


Wajumbe wa Baraza walieleza kuwa utekelezaji mzuri wa bajeti na kipaumbele kilichowekwa katika ulipaji wa stahiki umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza malalamiko ya watumishi, kuongeza ari ya kazi na kuimarisha ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa Wilaya ya Chalinze.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Baraza la wafanyakazi Chalinze lapitisha mapendekezo ya bajeti 2026/27

    February 10, 2026
  • Possi: Hakikisheni mnatokomeza sifuri kwa kusimamia ufundishaji Chalinze

    February 04, 2026
  • Kamati ya Mikopo ya Halmashauri yaketi kujadili maombi ya mikopo ya makundi maalum

    January 30, 2026
  • TRA yatambulisha Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Kodi (IDRAS)

    January 29, 2026
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.