• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Bilioni 2.5 Zapitishwa na Baraza la Madiwani Chalinze kwa ajili ya Matengenezo ya Barabara

Imewekwa: December 12th, 2023

                       Na John Mlyambate 

Madiwani wa Halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo wamepitisha rasimu ya Mpango wa Bajeti kwa mwaka 2024/2025 sh. 2.5 Bilioni iliyowasilishwa na Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini.


Fedha hizo ni mahitaji halisi kwa ajili ya matengenezo ya barabara huku nyingi zikiwa na malimbikizo ya matengenezo ambayo husababisha hali zake kuwa duni  na hivyo kuhitaji kiasi kikubwa cha fedha.


Kwa mujibu wa Meneja wa TARURA Wilaya ya Bagamoyo Mhandisi Bupe Angetile, mpango huo lengo lake ni kuondoa mapungufu ndani ya mtandao wa barabara unaosimamiwa na Taasisi hiyo kwa kutumia taarifa za utambuzi na hali halisi ya barabara.


Akiwasilisha rasimu hiyo kwenye kikao cha Baraza Maalumu la Madiwani Mhandisi Bupe alisema,  vigezo mbalimbali vimetumika wakati wa utayarishaji wa mpango huo ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa rasilimali fedha.


Vigezo vingine ni pamoja na mwenendo wa mahitaji ya uwekezaji, usalama wa warumiaji, aina ya barabara kwa misingi ya madaraja na tabaka la juu na wingi wa vyombo vya usafiri sambamba na kuboresha barabara za udongo kwenda Changarawe.


"Mapendekezo ya mpango huu wa bajeti 2024/2025 yanahusisha mpango kazi za mayengenezo inayogharamiwa na Mfuko wa barabara, pia miradi ya maendeleo ambayo hugharamiwa na mfuko huo na fedha za tozo za mafuta," alieleza Mhandisi Bupe.


Kadhalika alisema mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha 2023/2024 TARURA wilaya ya Bagamoyo katika Halmashauri ya Chalinze ilitengewa sh. 2.2Bilioni kutoka vyanzo vyote vya fedha ikiwemo mfuko wa barabara, tozo na fedha za Jimbo.


Hata hivyo hadi kufikia Novemba 2023, hakuna matumizi ya fedha za matengenezo ya miradi ya barabara kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Novemba kwakuwa hakuna mapokezi ya fedha za matengenezo.


Alieleza vikwazo katika Taasisi hiyo kuwa ni pamoja an ufinyu wa bajeti, uwepo wa miundombinu mbalimbali katika barabara zinazojengwa suala linalopelekea gharama za kuiondoa kuwa kubwa.


Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ramadhani Mkufya alisema TARURA wanatakiwa kuzingatia kuweka mifereji kwenye barabara wanazojenga ili zisiharibiwe kipindi cha mvua.


Diwani wa Ubena Godfrey Kamugisha aliomba Tarura kuwasimamia wakandarasi wajenge barabara imara kulingana na fedha zilizotolewa huku akiweka msimamo wa kutokubali fedha za matengenezo kupelekwa barabara ya Lulenge ambayo imejengwa chini ya kiwango badala yake zitumike kufungua barabara mpya ya Tukamisasa- Mbuyu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.