• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

CAMFED Yatoa Vishikwambi 477 kwa Shule za Sekondari Chalinze

Imewekwa: August 24th, 2018

Shirika la CAMFED Tanzania limetoa msaada wa vishikwambi 477 “e-Readers”katika shule za sekondari tisa katika halmashauri ya Chalinze,Vishikwambi hivyo vimetolewa hivi karibuni katika mashindano ya kuandika insha za kiingereza,kusimulia hadithi kwa lugha ya kiingereza na kongamano kwa lugha ya kiingereza katika shule ya sekondari ya Chalinze.

CAMFED ni shirika lisilo la kiserikali ambalo linashughulika na watoto wa kike wanaoishi katika mazingira hatarishi yanayowafanya washindwe kuendelea na masomo yao.Shirika hili lilianza kufanya kazi nchini Tanzania mwaka 2005 katika wilaya ya Iringa.Shirika hili limekuwa likishirikiana na serikali katika kumwezesha watoto wa kike kwenda shuleni kwa kuwalipia ada na mahitaji mbalimbali ya shule

Kwa sasa shirika hili linafanya kazi katika halmashauri tano za mkoa wa Pwani ambazo ni;Bagamoyo,Chalinze,Kibaha,Rufiji na Kibiti.Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa Camfed,Bi Latifa Sabuni katika hotuba yake alisema lengo kuu la mradi huu ni kuwawezesha watoto wa kike katika shule za sekondari wanawezeshwa kupata elimu kwa urahisi bila vikwazo kwa kuwapatia mahitaji ya msingi na kuwawezesha kutumia lugha ya kiingereza kwa ufasaha kupitia mashindano mbalimbali ya uandishi wa insha za kiingereza,usimulizi wa hadithi kwa lugha ya kiingereza na makongamano mbalimbali ya kuwajengea uwezo katika lugha ya kiingereza.Aliendelea kufafanua kuwa makongamano yatafanyika yataendelea kufanyika kwa ngazi ya shule na pia ushindani kati ya shule na shule ili kuimarisha stadi za lugha kwa wanafunzi.

Aidha Meneja Mradi wa mkoa wa Pwani alisema kama Camfed “tumeamua kutoa Vishikwambi 477 kwa shule tisa katika halmashauri ya Chalinze kwa maana kwamba kila shule imepata Vishikwambi 53,vishikwambi hivi vimehifadhi vitabu vyote vinavyotumika katika shule za sekondari kwa mujibu wa Mtaala wa serikali,shule zilizonufaika ni Kibindu,Kimange,Mandera,Kikaro,Msata,Kiwangwa,Lugoba na Chalinze.”Meneja Mradi alisema.

Kwa upande wake Meneja Rasilimali Fedha wa Mradi Bi Juli Tumbo aliwashauri na kuwaasa kutumia Vishikwambi walivyopewa katika kuimarisha stadi zao za Lugha kila wakati,aliendelea kuwatia moyo wanafunzi kwa kuwaeleza kuwa Elimu ni haki ya msingi kwa kila mtoto na lazima aipate ,ndiyo maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli aliamua kutoa elimu bila malipo kwa watoto wote wa Tanzania kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.”Hata sisi kama shirika tumeamua kuunga mkono Juhudi za serikali katika kutekeleza dhana ya Elimu bure lakini pia kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020 kama inavyojieleza”Tumbo alisema.

Naye mwakilishi wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Chalinze Christin Aidan alimshukuru Meneja Mradi na Uongozi wa shirika la Camfed kwa kuwapatia vitendea kazi vya kujifunzia yaani Vishikwambi”e-Readers”ambavyo vitakuwa msaada mkubwa katika kujifunza lakini pia alishukuru shirika kwa kuwezesha makongamano yanayoendelea katika shule zote katika halmashauri ya Chalinze.”Vishikwambi hivi vitakuwa msaada mkubwa kwetu sisi na walimu wetu katika kujifunza”Christin alisema.

Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Chalinze,Bwana Timothy Benard,ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji tuzo kwa wanafunzi walioshiriki katika mashindano ya stadi za lugha ya kiingereza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza,aliwasihi wanafunzi kujifunza lugha ya kiingereza kwa ufasha kwa kusoma vitabu mbalimbali vya lugha ya kiingereza ili kukuza msamiati na stadi za lugha lakini pia kuvitumia Vishikwambi ambavyo wamepatiwa na Camfed sanjari na kuwa na ushirikiano katika kujifunza kwa kuwa karibu na walimu katika kujifunza.”Kumbukeni Matendo ya leo ni Mafanikio ya Kesho”.Benard alisema.

Afisa Elimu aliendelea kuwasihi pia walimu wa masomo ya kiingereza wazidi kuwasaidia zaidi wanafunzi namna ya kujifunza somo la kiingereza kwani somo la kiingereza ni somo mama kwani ndiyo lugha ya kufundishia katika masomo yote yanayofundishwa sekondari.Timothy alilishukuru shirika la Camfed kwa jitihada kubwa za kuunga mkono serikali juu ya dhana ya elimu bure

Mwisho Afisa Elimu alimaliza kwa kutoa tuzo kwa washindi katika mashindano ya uandishi wa insha,masimulizi ya hadithi na kongamano kwa lugha ya Kiingereza.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.