• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Chalinze yapata Hati Safi mfululizo kwa miaka miwili

Imewekwa: July 3rd, 2019




Wataalamu wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wapongezwa katika kikao maalumu cha baraza la hoja za ukaguzi kwa mwaka wa Fedha 2018 /2019 kwa kazi nzuri wanazozifanya katika usimamizi na ukusanyaji mapato ya ndani na matumizi sahihi ya fedha kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za fedha.

    Pongezi hizo zimetolewa jana na wajumbe wa baraza la Madiwani, wataalamu kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali na wataalam kutoka sekretarieti ya Mkoa wa Pwani kwa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria za nchi na kupata Hati safi mfululizo kwa miaka miwili mwaka wa Fedha 2016/2017 na 2017/2018,hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) mweziAprili 2019.Taarifa hiyo ilionyesha hati ya ukaguzi,hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 pamoja na mapendekezo ya Mkaguzi kwa kila hoja iliyoibuliwa.

    Katika kikao hicho maalum Makamu Mwenyekiti Wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe Juma Mpwimbwi kwa niaba ya baraza la Madiwani aliwapongeza wataalam wa halmashauri kwakuzingatia sheria taratibu na kanuni katika matumizi ya fedha za halmashauri,na kwa kuwa wasikivu na waadilifu katika kupokea Ushauri na miongozo kutoka Mamlaka za juu kama sekretarieti ya Mkoa, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali."Matokeo ya uadilifu huo ni upatikanaji wa Hati safi mfululizo kwa miaka miwili."Mpwimbwi alisema.

     Kwa upande wake Afisa serikali za Mitaa kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Bwana Rashid Baghdellah aliupongeza uongozi wa halmashauri ya Chalinze kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za matumizi ya fedha kitu ambacho kimeiwezesha halmashauri kupata Hati safi mfululizo kwa miaka miwili. Baghdellah aliendelea kutoa Ushauri katika kuboresha ukusanyaji mapato kwa kutumia mbinu mbalimbali za kiteknolojia ili kudhibiti upotevu wa mapato, "Tumieni kamera maalumu (CCTV camera)katika vituo vya Malipo ya ushuru, kamera hizi zitatusaidia kupata uhalisia wa mapato tunavyokusanya ukilinganisha na Idadi ya malori yanayo pita kwa siku, kwa kufanya hivyo tutaongeza mapato ya halmashauri na kuimarisha ulinzi." Baghdellah alishauri.

    Diwani wa kata ya Kimange Mhe Hussein Hading'oka kwa furaha ya pekee aliwapongeza wataalam wa halmashauri kwa kuwa na ushirikiano mzuri katika kazi na Madiwani, wadau mbalimbali na wananchi kwa kitu kinacholeta ufanisi katika halmashauri ya Chalinze."Tumefanikiwa mengi kwa sababu ya umoja tulionao kati ya watendaji,madiwani na wananchi Chalinze tutazidi kushinda."Hading'oka alisema.

    Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Chalinze Bi Amina Kiwanuka alipokea pongezi hizo kwa niaba ya wataalam wa halmashauri na kupokea Ushauri wa wadau katika kuboresha shughuli za ukusanyaji mapato na utumiaji wa fedha za serikali kwa kuzingatia sheria za fedha za serikali za mitaa na bajeti kwa ujumla ili kuepukana na hoja za ukaguzi kwa kaguzi zijazo.

     





Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.