• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Chalinze yaunda timu ya UMITASHUMTA

Imewekwa: June 4th, 2018

Halmashauri ya wilaya ya Chalinze yakamilisha zoezi la uundaji wa timu ya wilaya ya Umoja wa Michezo na Taaluma wa Shule za Msingi Tanzania(UMITASHUMTA),kwa Mujibu wa Afisa Elimu Msingi Bi Zainabu Makwinya,”Mashindano haya yalinzia ngazi ya shule,Kata na leo tutahitimisha kwa kuunda timu ya wilaya itakayo peperusha bendera ya Halmashauri kwenda Mkoani kushindana na hatimaye kupata timu ya Mkoa”Makwinya alisema.

Makwinya aliyasema hayo katika taarifa yake ya uendeshaji wa michezo Jana katika viwanja vya shule ya sekondari ya Lugoba kwa Mgeni Rasmi katika mashindano hayo ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo,Mheshimiwa Majid Mwanga ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze,Bwana Edes Lukoa,Mwenyekiti wa Halmashauri,Mheshimiwa Said Zikatimu na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji,Mheshimiwa Malota Hussein ambaye ni Diwani wa kata ya Kiwangwa.

Afisa Elimu aliweza kubainisha changangamoto mbalimbali zinazoikabili Idara katika suala zima la uendeshaji michezo,ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti ya michezo unaaopelekea muda wa maandalizi kwa walimu na wanafunzi kuwa mfupi na kusababisha wanafunzi kutofanya vizuri katika mashindano wanapokuwa wanashindana na halmashauri zingine na ukosefu wa vifaa vya michezo.”Japo kwa mwaka huu hii siyo changamoto tena kwani mpaka sasa kwa bajeti ya mwaka huu wa fedha tumeweza kununua vifaa vya michezo vyenye thamani ya fedha za kitanzania Milioni 5.7 hivyo vifaa siyo tatizo tena kwa Chalinze na tutaendelea kuboresha kila mwaka.”Makwinya alisema.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri aliishukuru na kuipongeza Idara ya Elimu Msingi kwa moyo wa uzalendo wa kuweza kununua vifaa vya michezo pamoja na ufinyu wa bajeti na kuzitaka Idara zingine ziige na kujifunza kutoka Idara ya Elimu Msingi na kuwapongeza walimu kwa kujitoa kwao katika kuwaandaa na kuwasimamia wanafunzi kuanzia ngazi ya shule hadi ya wilaya na kusisitiza uadilifu kwa walimu na wanafunzi wanapokuwa katika kambi za michezo kwani uadilifu ni msingi wa mafanikio.

Naye mwenyekiti wa kamati ya Elimu,Afya na Maji,Malota Husein alisema “Kwa uzalendo mliuonyesha mimi pamoja na madiwani tutapambana katika kuboresha suala la michezo kwa kutenga bajeti inayotosheleza ili tuweze kuboresha michezo mashuleni,katika hili Mkurugenzi ,Mwenyekiti na madiwani kwa ujumla hatuna tatizo.”Malota alisema.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika shughuli hii muhimu alitoa nasaha zake kwa wanafunzi na walimu kwa kuwasisitiza kuzingatia maadili na sheria za michezo ili wapeperushe bendera ya Chalinze na kurudi na ushindi waendako na baada ya mashindano haya waje wasome kwa bidii kwa maslahi ya Taifa.Baada ya nasaha hizo alitamka rasmi kufungua mashindano hayo.




Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.