• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DC Bagamoyo Atatua Migogoro 28 Chalinze

Imewekwa: September 20th, 2018


Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Bi,Zainabu Kawawa,amesikiliza na kutatua migogoro 28 katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita.Mkuu wa wilaya ameanza kufanya kazi hii kama moja ya majukumu yake tangu alipoteuliwa hivi karibuni na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mheshimiwa Kawawa amekuwa akisikiliza na kutatua migogoro mbalimbali kama ya ardhi,mipaka ya mashamba,mifugo kulisha mashamba ya wakulima na migogoro mbalimbali ya kijamii katika halmashauri zake za Bagamoyo na Chalinze.


Aidha Mheshimiwa Kawawa amekuwa akiwatumia wataalam mbalimbali katika halmashauri zake kutatua migogoro Kama wataalam wa ardhi,wanasheria na wataalam wa maendeleo ya jamii,hii ni katika kuhakikisha kuwa sheria taratibu na kanuni zinafuatwa katika utatuzi huo na pale inaposhindikana suluhu huwashauri kufika katika vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.


Kwa mujibu wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Hamza Amri alitoa ufafanuzi kwa kusema Ofisi ya Mkuu wa wilaya imejipanga kusikiliza kero za wananchi kwa kusikiliza na kutatua kero kwa siku mbili kwa wiki kwa maana ya kila Jumanne ya wiki tunasikiliza na kutatua kero kwa halmashauri ya Bagamoyo na kila Siku ya Alhamisi ni siku ya kusikiliza na kutatua kero na migogoro kwa wananchi wa Chalinze, utaratibu huu unafahamika kwa wakurugenzi wa halmashauri zote mbili na wananchi wamekwisha fahamu juu ya kazi hii. Katibu Tawala alifafanua."Tumedhamiria kutatua kero za wananchi ili kutekeleza maelekezo ya serikali ya awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli."Amri alisema.


Naye Mzee Omari Salum mkazi wa kijiji cha Pongwemsungura kata ya Msata,aliyefika katika kituo cha kutolea malalamiko alitoa ushuhuda wake mbele ya mwandishi wa gazeti hilo kwa kumshukuru Mkuu wa wilaya kwa hatua zake za makusudi kuwasaidia wanachalinze na wanabagamoyo kwa ujumla."Mungu ambariki binti huyu kwa moyo wa kujitoa kututatulia migogoro yetu na kutupatanisha pale tulipotofautiana na huu ndiyo Uongozi tulioutaka."Mzee Omari alisema.


Kwa upande wake Bi.Harafa Mtaula mmoja wa mashuhuda waliotatuliwa kero zao alieleza kuwa."Mkuu wa wilaya huyu ni mshauri na Mwelekezaji katika kutatua kero na migogoro yetu,anatumia wataalamu wake katika kutatua migogoro na kuwaelekeza wataalam kuwashauri wananchi kwa mujibu wa kazi zao".Bi Harafa alisema.


Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo alitoa maelekezo kwa maafisa Tarafa wote katika wilaya yake kutembelea wananchi katika vijiji vyao na kutanzua migogoro iliyo ndani ya uwezo wao ili kupunguza msongamano wa siku za kutatua migogoro kwa ngazi ya wilaya.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.