• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

DC Kawawa akabidhi hundi ya milioni 338.3 kwa vijana na wanawake Chalinze

Imewekwa: March 1st, 2019




Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mheshimwa Zainabu Kawawa,amekabidhi hundi yenye thamani ya Fedha za kitanzania milioni 338.3 zilizotolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa vikundi 64 vya Vijana na wanawake kwa robo ya pili ya mwaka wa Fedha wa 2018/2019,Fedha hizo ni asilimia 10 ya Mapato ya ndani yanayo kusanywa na halmashauri hiyo makabidhiano hayo yamefanyika jana katika uwanja wa polisi Chalinze ,Mkuu huyo wa Wilaya katika hotuba yake ya kukabidhi hundi aliupongeza uongozi wa halmashauri ya Chalinze kwa kuheshimu na kutii maelekezo ya serikali kwa kutenga asilimia 10 ya Mapato ya ndani na kuwakopesha wanawake, vijana na walemavu.

      Hata hivyo Kawawa alihimiza ukusanyaji wa Mapato ya halmashauri kwa kuwataka wananchi na wataalamu kuziba mianya yote inayoweza kusababisha upotevu wa Mapato na kusababisha miradi mbalimbali ya maendeleo kutotekelezeka hivyo kukwamisha utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi. "Mikopo hii ya wanawake na Vijana itatekelezeka kwa sababu ya juhudi ya ukusanyaji wa Mapato inayoendelea, ndiyo maana miradi yetu katika maeneo mbalimbali inaendelea kutekelezwa. "Kawawa alisema.

     Akitoa ufafanuzi wa taarifa hiyo katika hafla ya ugawaji hundi kwa wanawake na Vijana, Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Bwana Shabani Millao alieleza kuwa robo ya pili ya mwaka wa Fedha 2018/2019 halmashauri imetoa kiasi cha shilingi milioni 338.3 ili kutekeleza bajeti na maagizo ya serikali ya kuwakwamua vijana na wanawake katika lindi la umasikini wa kipato kwa kuwakopesha asilimia kumi ya makusanyo ya Mapato ya ndani ya halmashauri. 

     Aidha Millao alieleza kuwa mpaka sasa takribani miaka mitatu tangu ianzishwe halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imekwisha toa mikopo kwa wanawake na Vijana  jumla ya Fedha za kitanzania milioni 967 kwa vikundi 257 na kuwawezesha Vijana na wanawake kujiajiri wenyewe kutokana na shughuli za ujasiriamali wanazozifanya kutokana na mikopo hiyo."Halmashauri ya Chalinze mpaka sasa haina deni lolote kwa upande wa Asilimia 10 ya Mapato ya ndani yanayo takiwa kupelekwa kwa wanawake na Vijana tunatekeleza kwa kadiri tunavyokusanya na kuisimamia bajeti kwa mujibu wa sheria." Millao alisema.

      Kwa upande wake Afisa maendeleo ya Jamii anayeratibu vikundi Bi Wahda  Mwishehe aliwataka wanawake na Vijana kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali  ili waweze kukopesheka kwa urahisi na kuwataka warejeshe mikopo kwa wakati ili mikopo hiyo waweze kukopeshwa na wengine. “ Akinamama wenzangu tuweni waaminifu kwa kurejesha mikopo mliyochukua kwa wakati kwani mambo yamekuwa rahisi kwa sasa kwani serikali imeondoa riba kwa wanawake na Vijana wanapokopeshwa na halmashauri. Mwishehe alifafanua.

    Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe Saidi Zikatimu alieleza kwa kina mafanikio ya halmashauri yake katika ukopeshaji fedha kwa vikundi vya wanawake na Vijana kwa kusema kuwa kwa halmashauri ya Chalinze kutoa mikopo siyo tatizo bali wanawake na Vijana kutounda vikundi kwa wakati ilikupatiwa mikopo hiyo,alitoa rai kwa maafisa maendeleo wa halmashauri kuwafikia wanawake na Vijana katika vijiji vyao na kuwapa Elimu ya namna ya kujiunga katika vikundi na kuwaelewesha mchakato mzima wa namna ya kupata mikopo,"Fedha tunazo tunahitaji Vijana na wanawake wajitokeze kuomba mikopo na mikopo hii haina riba kiasi cha Fedha atakachokopeshwa mlengwa ndicho atakachorudisha“. Zikatimu alieleza. 






Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.