• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Dkt Kalugila aiasa Jamii kuacha kutumia kemikali,sabuni na manukato sehemu za siri kuepuka magonjwa mbalimbali kama fangasi

Imewekwa: July 8th, 2024

Jamii imeaswa kutokutumia bidhaa zenye  kemikali kama sabuni,manukato na vileo hususani sehemu za siri ili kutunza afya zao na kuwa na utaratibu wakuvaa nguo zilizotengenezwa kwa malighafi ya pamba pia zisizo tunza joto litakalopelekea unyevu mwilini ili kuepukana na magonjwa mbalimbali ikiwemo fangasi sehemu za siri kwa mwanamke.

Dkt  Philemoni Kalugila ameyasema hayo  leo Julai 02 ,2024 alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha Chalinze fm kwenye kipindi cha Gumzo leo kinachoruka Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 04:00 asubuhi hadi saa 07:00 mchana kwa lengo la kutoa elimu ya afya kwa jamii. 

Aidha Dkt Kalugila  amesema fangasi ni vijiumbe wanaopatikana kwenye mwili wa binadamu kuanzia kwenye mdomo hadi njia ya haja kubwa katika  uwiano mzuri na kwa mazingira ya ukeni fangasi aina ya vaginal candidiasis katika kundi la fangasi wanaoitwa candida albicans wanapokuwa kwa wingi ndio huleta shida mwilini na kusema kuwa wenye changamoto ya ugonjwa wa kisukari wanapaswa kudhibiti mazingira ya sukari mwilini inayopeleleka bakteria kuzaliana kwa wingi ili kupunguza uwezekano wa tatizo la fangasi kujirudia.

Vile vile Dkt Philemoni ametaja mazingira yanayopelekea tatizo hilo ni kupungua kwa kinga za mwili zinazosababishwa na  maradhi kama HIV,tb na matumizi holela ya dawa kama antibiotic, steroids kwa watu waliopandikizwa viungio,wenye aleji zinazoshusha kinga za na kusisitiza kwa na utunzaji wa uke kwa kusafisha kwa maji safi na kutokutumia  sabuni,manukato wala pombe kali  kwa kuweka ukeni na kwenye njia ya haja kubwa hususani kwa baadhi ya vijana na wanafunzi ili asiweze kusikika wanatoa harufu ya pombe mdomoni wa kutumia inapelekea kubadili mazingira na fangasi wanazaliana kwa wingi na kuleta adhari na kuleta ugonjwa,mabadiliko ya homoni katika mwili,

Akizitaja dalili kuu za fangasi sehemu za siri kwa mwanamke Dkt Philemon amesema ni pamoja na kuhisi kuwashwa,kuwa na hali ya ukavu sehemu za siri kutokwa na vidonda,kutokwa na uchafu mweupe ulioganda kama maziwa,kupata maumivu wakati wa  haja ndogo na pia wakati wa kushiriki tendo la ndoa.Pia amewashauri  wanaoshiriki mapenzi kwa njia ya mdomo na kuacha mara moja ili kuepukana  kupata maambukizi ya magonjwa kwani si njia salama.

Sanjari na hayo Dkt Kalugila ametaja madhara mtu anayoweza kuyapata  ni changamoto  kwenye viungo vya uzazi mfumo wa uzazi na ametoa wito kwa jamii kujitokeza  kwa wingi kwenye vituo vya afya na Hospitali zilizo karibu nao ili kupima na kuanza tiba mara moja pindi wanapokutwa na changamoto za kiafya.

Pia Dkt  Kalugila ametaja  faida za fangasi mwilini  ni kuleta ulinzi na wanapozaliana kwa wingi ndio husababisha  ugonjwa na kusema kuwa takwimu  zinaonyesha asilimia 70% wanawake wamewahi kuugua fangasi kwenye maisha walau mara moja katika kipindi cha maisha yao na 50% wamewahi kuugua walau mara mbili pia  wajawzito hukumwa na changamoto hiyo kutokana na mabadiliko makubwa ya homoni na umri hasa walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu ni kati ya miaka 15 hadi 49.

Daktari ametoa wito kwa jamii wito kuwa na mazoea ya kununua bidhaa zenye ubora na sehemu zinazo aminika ili kuendelea kutunza afya zao pia kutokukaa  na na kuvaa nguo zenye unyevunyevu ukeni mara baada ya kutoka kuogelea au kufanya mazoezi.

 

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.