• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Dstv na UN Global Compact wagawa Miche 2000 ya Miti Chalinze

Imewekwa: January 23rd, 2023


Dstv kwa kushirikiana na Asasi isiyo ya kiserikali ya UN Global Compact Network Tanzania wametoa miche kwa ajili matunda na biashara ipatayo 2000 katika Halmashauri ya wilaya ya Chalinze makabidhiano hayo yamefanyika jana katika viwanja vya shule ya msingi Bwilingu A .Wakikabidhi Miche hiyo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete ili aweze kuzikabidhi shule za Msingi na Sekondari zipatazo 10, Mkurugenzi wa UN Global Compact Bi.Marsha Macatta-Yambi alieleza dhima kuu ya Taasisi yake ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika suala zima la utunzaji wa mazingira nchini Tanzania.


Bi. Macatta-Yambi ameahidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Chalinze katika suala zima la utunzaji Mazingira sanjari na kutoa miche zaidi katika Taasisi za serikali kama shule na taasisi zingine ambazo zitakuwa tayari kupanda na kuitunza miti hiyo.


Shule zilizopatiwa miche hiyo ni Shule za Msingi 6 ambazo ni Bwilingu A,Bwilingu B, Kibiki,Msoga,Chalinze na Chalinze Islamic. Kwa upande wa shule za sekondari ni Chahua,Beracha Valley,Moreto na Msata.


Mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi miche hiyo Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete(Mb) na Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi alizipongeza Taasisi za Dstv na UN Global Compact kwa uamuzi wao wa kugawa miche 2000 katika Halmashauri ya Chalinze na kuwaomba waendelee kusaidia na kuunga Mkono jitihada za serikali katika kuyatunza mazingira na kutoa Elimu zaidi ya utunzaji Mazingira kwa wananchi, kwani kupitia utunzaji wa mazingira kutakuwa na mvua za uhakika katika maeneo yetu hivyo kuwa na uhakika wa chakula kwa wananchi wetu.


Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alitoa rai kwa taasisi zingine pia kuunga mkono jitihada za serika katika suala la utunzaji mazingira ,alizitaka taasisi za fedha kama mabenki yanayofanya kazi katika halmashauri ya Chalinze kuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha wananchi wayatunze mazingira sanjari na utoaji wa miche ya kupanda.


Aidha Naibu waziri aliwaomba wananchi kuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira ili mazingira yawatunze.

“Ndugu wananchi nawaomba tuwe na utamaduni wa kupanda miti kila familia kwani jukumu la kuyatunza mazingira ni jukumu letu sote kwa faida yetu na vizazi vijavyo.” Naibu Waziri alisema.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze,Mheshimiwa Hassani Mwinyikondo alizipongeza taasisi za Dstv na UN Global Compact kwa kuwa wazalendo wa kweli kwa kuunga mkono Juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuyatunza na kuyalinda mazingira,pia aliziahidi taasisi hizo kuzipatia ushirikiano wa hali ya juu katika kuboresha mazingira katika halmashauri ya Chalinze.


Kwa upande wake Meneja wa benki ya CRDB Kibaha, Bi Rose Kazimoto aliahidi kutoa ushirikiano mkubwa katika kuyalinda na kuyatunza mazingira kupitia taasisi yake,pia aliwaahidi wananchi upatikanaji wa huduma za kibenki kupitia taasisi yake muda si mrefu kuanzia sasa kwani wapo hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa benki tawi la Chalinze.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.