• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Elimu Dhidi ya Kichaa cha Mbwa yatolewa Chalinze

Imewekwa: September 28th, 2022

Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze yaadhimisha Siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani

Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze  leo imeadhimisha siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani katika viwanja vya shule ya Msingi Chalinze kata ya Pera kwa kutoa elimu kwa jamii na wanafunzi kuhusu ugonjwa huo pamoja na kutoa chanjo bure kwa mbwa na paka.

Maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka yamefunguliwa rasmi  na Mhe.Nasser Karama Diwani wa kata ya Bwilingu kwaniaba ya Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Chalinze ambapo amesema kuwa ni mafanikio makubwa kwa Serikali na Halmashauri kwa kuandaa maadhimisho hayo kwa kutoa  elimu ya kichaa cha mbwa kwa wanafunzi kwani itawasaidia kuchukua tahadhari ili kuepukana na kichaa cha mbwa.

“ Maadhimisho haya ya kichaa cha Mbwa Duniani ni mafanikio makubwa kwa Serikali na Halmashauri kwa ujumla kupitia idara ya mifugo kwa kuandaa maadhimisho haya shuleni kwani hatari nyingi na madhara ya kichaa cha mbwa yanawakumba sana vijana wetu waliopo mashuleni hivyo basi elimu iliyotolewa hapa itawasaidia wanafunzi na jamii kwa ujumla kujikinga na madhara haya ya ugonjwa”. Amesema Mhe.Nasser.

Hata hivyo Mhe Nasser aliendelea kwa kuwaasa wananchi kuwaleta mbwa wao katika maadhimisho hayo nakuwa na utaratibu wa kuwapatia wanyama hao chanjo ili kuilinda jamii dhidi ya kichaa cha mbwa kwani kufuga mbwa ni hiari bali kumpatia chanjo ni lazima.

Aidha kwaniaba ya wananchi wa Kata ya Pera Diwani wa kata  hiyo Mhe.Jackson Mkango amesema kuwa wananchi wa kata ya  Pera wamepata uelewa mkubwa juu ya kichaa cha mbwa pamoja na kutambua kuwa jukumu la utunzaji wa mbwa kwa mfugaji ni lazima.

“Kwaniaba ya wananchi wa kata ya Pera tunaishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa kuichagua kata yetu ya Pera kuwa  sehemu ya kutoa elimu kwenye maadhimisho haya na pia tumepata kujua kuwa ufugaji wa mbwa ni hiari lakini kwa miongozo ya serikali utunzaji wa mbwa hasa kuwapatia chanjo ni lazima”,Amesema Mhe. Mkango.

Nae Afisa Mifugo wa Halmashari ya Wilaya ya Chalinze Ndg.Msongo Songoro ameelezea lengo kuu la maadhimisho haya ya Kichaa cha mbwa Duniani kwa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ni kuipa jamii elimu juu ya kuwatunza vyema mbwa na paka pamoja na namna ya kujikinga na mbwa ambao wanaweza kuhatarisha afya kwa jamii.

“Lengo la maadhimisho haya ni kuipa jamii elimu kwa kutunza mbwa na paka vizuri pamoja na kuwahudumia ili wasiweze kupata ugonjwa huu kwani mbwa na paka wakipata ugonjwa huu wanaweza kuleta maambukizi ya kichaa cha mbwa kwa binadamu endapo atang’atwa na mbwa aliyeathirika”Amesema Ndg.Msongo

Vilevile ndugu Msongo amewataka wananchi wanaofuga wanyama hao  kuwafikisha katika ofisi za kata ili waweze kupatiwa chanjo bila malipo.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Dkt Kikwete ahakiki taarifa zake Daftari la kudumu la mpiga kura Msoga

    May 16, 2025
  • Chalinze yatoa mafunzo ya wagawa Dawa za Kinga tiba dhidi ya mabusha na matende

    May 16, 2025
  • Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Chalinze Afungua mafunzo ya waandikishaji

    May 15, 2025
  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.