• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Chalinze na Ruangwa yaanzisha urafiki wa kikazi.

Imewekwa: February 9th, 2022

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na Halmashauri ya Ruangwa wameanzisha uhusiano na urafiki wa kikazi ikiwa na lengo la ushirikiano katika sekta mbalimbali za kimaendeleo baina ya Halmashauri hizo mbili.

Hayo yametokana na ziara fupi ya Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe.Endrew Chikomwe na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Mhe. Hassan Mwinyikondo  na wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili wamekubaliana  kuanzisha ushirikiano huo hata kwa maandishi ili kuleta maendeleo katika Halmashauri hizo.

Ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ruangwa Mhe.Endrew Chikomwe amewaeleza baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Chalinze kuwa ushirikiano utaibua maendeleo Zaidi baina ya Halmashauri hizo,

“ Kwaniaba ya Halmashauri ya Ruangwa Nimezungumza na Mwenyekiti Mwenzangu na Mkurugenzi kuanzisha urafiki huu baina ya Halmashauri zetu utakaolenga kufanya na kupanga mikakati ya kimaendeleo katika sekta mbalimbali katika Halmashauri zetu hizi na pia kujifunza kwa kila mmoja wetu pale ambapo amefanikiwa jambo”. Alisema Mhe. Chikomwe.

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ruangwa Ndg. Frank Chonya ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa kuwa na jingo zuri pamoja na ukumbi na kuahidi kujifunza kupitia Halmashauri hiyo

“Kwanza tumefurahi kufika hapa Chalinze  na tumefurahishwa jinsi mlivyotupokea mimi na Mheshimiwa Mwenyekiti wangu , na niwapongeze kwa kuwa na jingo zuri sana na ukumbi uliopangiliwa vizuri basi nasi tumejifunza ni kwa namna gani tutapangilia jengo letu jipya.” Alisema Ndg.Chonya.

Kwa upande wa Halmashauri ya Chalinze kupitia Mwenyekiti wake Mhe.Hassan Mwinyikondo ameahidi ushirikiano mkubwa baina ya Halmashauri ya Chalinze na Halmashauri ya Ruangwa ,

“Kwa niaba ya Halmashauri ya Chalinze niseme kuwa tumefurahishwa na ujio wenu hapa kwetu na tunaahidi kuwa na ushirikiano mkubwa baina yenu na yetu kwani itasaidia kuleta maendeleo kwenye Halmashauri zetu na Taifa kwa ujumla kwa kujifunza pale walipofanikiwa wenzetu.” Alisema Mhe. Mwinyikondo.

Mhe. Mwinyikondo ameongeza kwa kuwataka baadhi ya maafisa wa idara  wa Halmashauri ya Chalinze kufanya ziara ya kujifuza yale mazuri katika Halmashauri ya Ruangwa ikiwepo idara ya kilimo pamoja na idara ya Elimu yaani Elimu Msingi na Elimu sekondari.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.