• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Chalinze yafanya vikao vya Mafunzo ya kuboresha mikakati ya Elimu Nchini

Imewekwa: September 10th, 2022

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze yafanya vikao vya mafunzo ya uwasilishaji wa miongozo ya mikakati ya kuboresha elimu nchini.

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kupitia Idara ya elimu msingi  pamoja na idara ya elimu sekondari zimekutana katika shule ya sekondari Lugoba na kufanya vikao vya mafunzo ya uwasilishaji wa miongozo ya elimu na walimu wa kada hizo kwa nyakati tofauti ambapo miongozo hiyo iliyowasilishwa ni pamoja na muongozo wa uteuzi wa viongozi wa elimu,Muongozo wa mikakati ya ufundishaji kwa shule za msingi na sekondari na muongozo wa nini kifanyike katika kutatua changamoto zilizopo.

Vikao hivyo viwili tofauti vimehudhuriwa na Maafisa elimu Wilaya,Wadhibiti ubora,Afisa kutoka Tume ya utumishi wa walimu,Maafisa elimu kata pamoja na walimu wakuu wa shule za sekondari na msingi.

Kikao hicho kilianza tangu siku ya tarehe 08/09/2022 ambapo idara ya elimu sekondari ndio walianza kikao hicho kilichoongozwa na Afisa Elimu sekondari Mwl. Salama Ndyetabura ambapo katika kikao hicho Afisa elimu huyo amesema kuwa kikao kimekuwa cha mafanikio kwani washiriki wapokea miongozo hiyo kwa furaha na kuahidi kuifanyia kazi

“Kikao hiki cha leo kimekuwa cha mafanikio kwani washiriki wote wameonesha kupokea miongozo hii kwa furaha na kuahidi kuanza kuifanyia kazi hasa wamefurahia kuwa wanakwenda kufanya kazi wakiwa na miongozo lakini pia wamefurahia maelekezo waliopewa na wadhibiti ubora juu ya kupima umahiri na jinsi ya kutoa taarifa zao wanapokuwa wanafanya ufuatiliaji”. Amesema Mwl. Ndyetabura

Vilevile ameongeza kwa kusema kuwa kama Halmashauri imeweka mikakakati ya kufanya ufuatiliaji ambapo Halmashauri kupitia idara ya elimu Sekondari imegawa walezi katika kila shule na wadhibiti ubora wakisaidiana na maafisa elimu kata katika ufuatiliaji na piaafisa elimu huyo amepanga kufanya kikao kwa siku tano na walimu wanaofundisha madarasani ili waweze kusikia na kuyaelewa maelekezo.

Aidha siku ya tarehe 09/09/2022 idara ya elimu msingi  kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze imeweza kukutana pia nakufanya kikao na walimu wa shule za msingi ambapo ufunguzi wa kikao hicho umefanywa na Afisa elimu msingi Mwl.Miriam Kihiyo ambapo katika kikao hicho afisa elimu amesema kuwa miongozo hii imewasilishwa kwa walimu wakuu ili waweze kuwawasilishia walimu wenzao mashuleni.

“Miangozo hii imewasilishwa kwa walimu wakuu ili walimu hao waweze kuwawasilishia walimu wenzao mashuleni ili walimu nao waweze kuifuatilia miongozo hiyo na kuweza kuboresha elimu na pia tumewafikishia walimu kwasababu ndio walengwa na pia ndio wanaokaa na watoto ndio wanawasimamia watoto kujua kusoma,kuhesabu na kuandika”. Amesema Mwl. Kihiyo.

Mwl. Kihiyo ameendelea kwa kusema kuwa kwa kutoa mafunzo ya miongozo hii watakwenda kubadilisha ufundishaji na kutengeneza matokeo mazuri kwa watoto wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze,Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Nae  Naibu Mdhibiti Mkuu Ubora wa Shule Chalinze Bi. Grace Bwali amesema kuwa ofisi ya uthibiti ubora itahakikisha wanafanya ufuatiliaji kwa kila shule ili kuona na kutoa ushauri ili kuweza kuinua taaluma.

“Kwa upande wetu tutahakikisha tunaweka utaratibu madhubuti wa kufuatilia kila shule ili kuona miongozo hiyo inavyofanyiwa utekelezaji na kutoa ushauri madhubuti ili kuhakikisha kile walichofundishwa na kila ambacho tunawaongezea kinakwenda sawa ili kuweza kuinua taaluma ya Halmashauri yetu ya Wilaya ya Chalinze”.Amesema Bi Grace.

Vilevile tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Bagamoyo na Chalinze imewakilishwa na Nd.Sadick Rajabu ambapo kwa upande wao wameahidi kjuendelea kusimamia suala zima la nidhamu na maadili ya kazi ya ualimu kwa walimu wote.

“Kwa upande wetu ili kuhakikisha mafunzo ya miongozo iliyotolewa leo inafanyiwa kazi tutasimamia katika suala zima la nidhamu kwani tutaweka nguvu zetu kwa walimu wakuu hawa ili kuzingatia suala la nidhamu na maadili kwa walimu wao na kuhakikisha anasimamia niddhamu kama mamlaka aliyopewa yanavyoeekeza”. Amesema ndg. Sadick.

Kwaniaba ya walimu wakuu waliohudhuria kikao hicho maalum Mwl. Adinan Issa kutoka Shule ya Msingi Mdaula amesema kuwa amayapokea vyema mafunzo hayo na kilichobaki ni kutoka kwao katika utekelezaji.

Kiukweli mafunzo yalikuwa katika mtirirko mzuri na ni vitu vipya ambavyo vinahitajika kufahamika kwa walimu kwasababu ya kiutendaji na tumejifunza vitu vingi hasa katika uendeshaji wa shule na kilichobaki kutoka kwetu ni utekelezaji”.Amesema Mwl. Adinani

Ikumbukwe kuwa uwasilishaji wa miongozo hiyo Kitaifa ilizinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Mkoani Taboraa tarehe 04/08/2022.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.