• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Chalinze yapata mgao wa Zaidi ya Bil 1.6

Imewekwa: October 22nd, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ni moja kati ya Halmashauri 184 za Tanzania Bara ambazo zimebahatika kupata kiasi cha fedha Shilingi Bilioni 1.68 kutoka katika sehemu ya shilingi bilioni 535.68 ambayo ni asilimia 41.1 zilizoelekezwa katika Wizara ya TAMISEMI zilizotokana na mkopo wenye masharti nafuu wa Shilingi trilioni 1.3 za Kitanzania  kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 ili kuchangia kufufua uchumi kwa Sekta zilizopata athari za kiuchumi kutokana na madhara ya UVIKO-19 nchini Tanzania.

Akizungumza kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mwenyekiti wa kikao hicho cha utekelezaji Ndg Shabani Millao ambaye ni Afisa Mipango, Tkwimu na Ufuatiliaji (W) alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada zake za kupata fedha hizi na alifafanua mchanganuo wa miradi ambayo itafikiwa na fedha hizo.

“ Nipende kumshukuru Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake na upendo wake kwa Watanzania mpaka kupata fedha hizi kwa maendeleo ya wanaChalinze na Watanzania kwa Ujumla, Halmashauri ya Chalinze  imepokea kiasi cha Shilingi Bil 1,680,000,000/= ikiwa gharama na maeneo yafuatayo yatafikiwa ikiwemo shilingi 1.320,000,000/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 66 katika shule za sekondari ili kuweza kupokea wanafunzi wote wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2022 ambavyo ndivyo vilivyokuwa uhitaji halisi kwa Halmashauri yetu. Ujenzi wa madarasa huo unaenda sambamba na utengenezaji wa viti na meza kwa vyumba vyote ambavyo vitafikia idadi ya 3300, pia shilingi 280,000,000.00/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 14 kwa shule (vituo) shikizi vitano na shilingi 80,000,000/= itatumika kwa ajili ya ujenzi wa Bweni la watoto wenye mahitaji maalumu kwa shule ya msingi Chalinze”.Alisema Ndg. Shaban Milao.

Aidha  katika taarifa ya Mpango huo Halmashauri imepatiwa mgao wa magari mawili moja likiwa la gari ya Wagonjwa na gari la usimamizi wa huduma za Afya na imepata mgao wa Mashine moja ya Mionzi (X-Ray) ambayo itatumika kusaidia kutoa huduma katika Halmashauri ikiwa na thamani ya Shilingi 420,000,000/=

Kikao hicho cha mkakati wa utekelezaji kimehudhuriwa na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze pamoja na wakuu wa shule mbalimbali zilizopo katika Halmashauri ya Chslinze.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.