• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Wilaya Chalinze yafanya Dua kumuombea Hayati Dkt John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Imewekwa: April 7th, 2021

Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya Chalinze chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Geofrey Kamugisha na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Ramadhani Possi kwa kushirikiana na Kamati ya Amani ya wilaya ya Bagamoyo tarehe 07.04.2021 katika ukumbi wa Halmashauri wamefanya maombi maalumu kwa ajili ya Kumuombea alikuwa Rais wa Jamhuli ya Mungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Kamugisha aliwashukuru wajumbe wote ambao ni viongozi wa Dini ya Kikristo na Kiislamu kwa kufika kwao na kuwaelezea adhima ya hafla hiyo. Mwenyekiti alisema,"Napenda kuwashukuru sana sana wajumbe wote kwa kufika kwenu, lengo kubwa la sisi kukutana hapa ni kufanya maombi maalumu kwa ajili ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ili Mungu amrehemu na kumuhepusha na adhabu ya mauti. Sio hivyo tu bali na kumuombea Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan ili Mungu ampe nguvu, Ujasiri, Amani na Uwezo katika kutekeleza majukumu yake ya Urais alioupokea.


Aidha, Mhe. Kamugisha aliongeza kusema, "Halmashauri ya Chalinze itaendelea kumuenzi Hayati John Pombe Magufuli kwa vitendo kwa kufanya kazi na kutekeleza miradi mikakati yote ambayo ilianzishwa na Halmashauri ya Chalinze katika awamu yake, na kusimamia rasilimali za wananchi ili kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya Chalinze na Taifa kwa ujumla.


Mhe. Kamugisha alihimiza viongozi wa dini kuendelea kuhamasisha Amani ndani ya Chalinze na Taifa kwa ujumla ili nchi iwe salama kwa wananchi na wawekezaji kuishi. Alisema, "Ndugu wajumbe wa hafla hii na Kamati ya Amani ya Wilaya (viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo pamoja na waumini wao) napenda kutoa wito kwenu kuendelea kuhamasisha Amani, Upendo na mshikamano kwa waumini wenu muwapo katika ibada  ili kuongeza kasi ya kulijenga Taifa lenye utulivu. Mhe. Kamugisha aliongeza, "Kama viongozi tunapenda kuwahakikishia kuwa kazi zinaendelea hata baada ya kuondokewa na Aliyekuwa Rais Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuwa sasa tunaye Rais Imara ba Shupavu Mh. Samia Suluhu Hassan. Kikubwa tuzidi kumuombea ili yale yote mema ambayo Mungu amekusudia tuyapate kupitia yeye basi yakafanyike kwa wakati".


Alisema Halmashauri inaendelea na Utaratibu wa uimarishaji wa vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na uibuaji wa vyanzo vipya na uendelezaji wa Miradi mikakati kama Ujenzi wa Stadi, Soko, Sehemu ya maegesho ya Magari Makubwa, Ujenzi wa kumbi za mikutano au sherehe na Ununuzi wa Greda ili kufungua barabara kuchangia katika jitihada za TARURA. Na kuwa hivyo vyote vina lengo la kuongeza pato la Halmashauri na kusaidia katika utekelezaji wa Mambo mengi ya kimaendeleo ambayo yatagusa maisha ya mwanachalinze mmoja mmoja.


Naye Mwenyekiti wa kamati ya amani kwa niaba ya viongozi wa dini Ndg. Alhaji Khamis Nassoro alisema Hayati Magufuli alikuwa ni kiongozi wa mfano kwani alifanikiwa kuunganisha watu wa dini zote. Katika kipindi cha uongozi wake, hapakuwahi kutokea hata migogoro ya kidini baina ya Wakristo na Waislamu. Pia, alisema yapo mambo mengi aliyowaahidi wanachalinze ikiwemo uboresha wa miundombinu ya maji, barabara, Masoko na Viwanda na kuifanya Chalinze iwe kama Singapore jambo ambalo halikukamilika mpaka mauti yanamfika. "Tuna imani na Rais aliopo madarakani Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa ataendeleza pale alipoishia Hayati Dkt. Magufuli".


Aliwataka wananchi wa Chalinze kuendelea kuishi maisha ya kumtumaini Mungu na kuzidisha dua kwani ndio njia pekee itakayowaweka tayari kufika mwisho mwema wa maisha yao katika dunia hii. Katika kuhitimisha Ibada hiyo maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dr. John Pombe Magufuli, Rais wa sasa Mhe. Samia Suluhu Hassan na Halmashauri ya Wilaya Chalinze iliyoendeshwa na viongozi wa dini wa pande zote yaani Wakristo na Waislamu, viongozi hao walimuomba Mungu kumpa pumziko la amani Hayati Magufuli na kumuombea Afya njema, hekima, Upendo na Uvumilivu Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan ili aweze kuiongoza vema Tanzania na kuzidisha kasi ya ukuaji wa kiuchumi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.