• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge azindua rasmi CHALINZE JOGGING CLUB.

Imewekwa: October 9th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge hii leo amezindua rasmi (Chalinze Jogging Club) katika bonanza lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Chalinze na Halmashauri ya Chalinze.

Akizungumza mara baada ya Shughuli ya uzinduzi Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa  amewashukuru watendaji wa Chalinze kwa kuanzisha umoja huu kwani unatengeneza mahusiano mazuri.

“ Nimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Abdallah kwa kushirikiana na Mbunge wetu Mhe. Ridhiwani Kikwete, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Ismail Msumi pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Ndg. Ramadhan Possi kwa kunipa heshima ya kuzindua (Chalinze Jogging Club) iliyopo Chalinze na tumepata wasaa wa kukimbia takribani kilomita 3 kutoka Ofisi za Halmashauri mpaka viwanja vya polisi na tukio hili linaakisi tamaduni za kitanzania za kujenga undugu na mahusiano mazuri kwa jamii na taasisi mbalimbali ambazo tunashirikiana nazo na pia hii ni kama muendelezo wa kauli ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutenga siku maalumu kwaajili ya kufanya mazoezi” Alisema Mhe. Abubakar Kunenge.

Vilevile Mhe. Kunenge amewaasa Wanachalinze kuendelea kupenda kufanya mazoezi na pia kujikinga na Ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kutumia vitakasa mikono, kunawa na maji tiririka  pamoja na kupata Chanjo ya UVIKO-19 kwani hata leo hii katika viwanja hivi  chanjo hiyo inatolewa bila malipo yeyote.

Aidha Mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kuweza kufanikisha tukio hili kubwa la uzinduzi na kuwaomba waandishi wa Habari kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Chalinze katika kutangaza miradi mbalimbali iliyopo Chalinze.

“ Kwanza nipende kumpongeza Mkuu wetu wa Mkoa wa Pwani kwa kushiriki nasi katika tukio hili kubwa na pia pongezi kwa mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kwa kuweza kufanikisha tukio hili, kwani tukio hili ni kubwa na ni muhimu kwa kujenga undugu na Afya kwa ujumla na pia nawaomba ndugu waandishi wa habari muendelee kumuunga mkono Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya na Halmashauri ya Chalinze kwa kuitangaza Chalinze kupitia miradi mikubwa iliyopo ndani ya Halmashauri yetu ya Chalinze”. Alisema Mhe. Ridhiwan Kikwete(Mb).

Nae Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Abdallah amewatangazia wananchi nchini kote kuwa kutakuwa na tamasha la kimataifa la Sanaa na Burudani litakaloanza Tar. 28/10/2021 mpaka 30/10/2021 katika Wilaya ya Bagamoyo.

“ Ninawatangazia rasmi Watanzania wote  kuwa Tar. 28/10/2021 mpaka 30/10/2021 kutakuwa na Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Burudani ambalo linasimamiwa na Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo, hivyo basi nawaalika watanzania kwa ujumla kujumuika nasi katika Wilaya yetu ya Bagamoyo ili kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya Wilaya yetu ya Bagamoyo.

Hata hivyo Mhe. Zainabu Abdallah amewaalika Wanachalinze kujumuika katika muendelezo wa bonanza hilo la uzinduzi wa (Chalinze Jogging Club) ambapo uzinduzi huo unaambatana na Kukabidhi vifaa katika shule ya Msingi Chalinze(Pera) kwa watoto wenye mahitaji maalumu pamoja na Kutembelea Wodi ya kina mama katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliopo katika Kata ya Msoga, Katka bonanza hilo Michezo mbalimbali kama Mpira wa miguu, ngoma za kitamaduni na Mkesha wa burudani ya muziki vitafanyika kuhakikisha wanachalinze wanapata Burudani kwa ukamamilifu,

Mkuu wa Mkoa .Mhe. Abubakar Kunenge(wakatikati Mrefu) akiwa na Viongozi wa Wilalaya ya Bagamoyo na Halmashauri ya 

Chalinze katika bonanza la Uzinduzi wa Chalinze Jogging Club



Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.