• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

JUMA LA ELIMU LIWE CHACHU NA KICHOCHEO CHA MAENDELEO YA TAARUMA KWA HALMASHAURI YA CHALINZE

Imewekwa: May 9th, 2017

Maadhimsho ya juma la elimu Halmashauri ya Chalinze yafanika katika viwanja vya shule ya msingi Msata.Katika maadhimisho hayo Afisa elimu Msingi Bi Zainabu Makwinya

akizungumza katika sherehe hizo alisema

''Ndugu Mgeni Rasmi,

Tunayo mafanikio mbalimbali ya kielimu yaliyopatikana kwa miezi 11 ya utendaji kama Halmashauri. Mafanikio hayo yamefikiwa kutokana na ushirikiano mzuri uliopo miongoni mwetu na jamii inayotuzunguka. Pia ushirikiano na msaada mkubwa tunaoupata kutoka kwa waheshimiwa wabunge, waheshimiwa madiwani, ofisi ya mkuu wa wilaya kwa ujumla wake na wadau wengine katika sekta hii. Mafanikio hayo ni kama ifuatavyo:-

•Kusogeza huduma karibu kwa wadau wote wa Elimu ikiwemo wanafunzi, wazazi, walimu, mashirika mbalimbali.

•Kuwezesha kuondoa wanafunzi hewa kwa kuwasajili kupitia mfumo wa kuhifadhi taarifa za wanafunzi  (PReM na BEMIS).

•Idara ya Elimu Msingi imeweza kuandikisha wanafunzi wa awali 4,363 Ambao wavulana ni 2,147 na wasichana ni 2,216 Darasa la kwanza 10,350 kati yao wavulana 5,338 na wasichana 4,967 kwa mwaka 2017.

•Kuongeza ufaulu wa wanafunzi wanaomaliza Elimu ya Msingi kwa asilimia 99.7. Kwa mwaka 2016 jumla ya wanafunzi 4,029 walifanya mtihani wa kuhitimu Elimu ya Msingi wakiwemo wasichana 2,213 na wavulana 1,816. Jumla ya wanafunzi  2,511 walifaulu na kuchaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka 2017 wakiwemo wasichana 1,308 na wavulana 1,203 ambapo ni sawa na ongezeko la 1% ukilinganisha na wanafunzi 2,469 wakiwemo wasichana 1,365 na wavulana 1,104 kwa mwaka 2016 waliofikisha alama za kuchaguliwa kujiunga na Elimu ya Sekondari.

•Kuwezesha kupatikana wa ufaulu wa mitihani ya Taifa kwa kidato cha Pili kwa asilimia 91%  kwa mwaka 2016 ambapo wanafunzi 2,225 wakiwemo wavulana 1,035 na wasichana 1,190 waliotahiniwa walifaulu kwa asilimia 91%  kwa daraja la 1-4 na asilimia 9 ambayo ni wanafunzi 210 wakiwemo wavulana 84 na wasichana 126 hawakufikia vigezo hivyo kukariri kidato. ●Kupandisha ufaulu wa mitihani ya Taifa kwa kidato cha Nne kwa mwaka 2016 ambapo wanafunzi 1775 wakiwemo wavulana 858 na wasichana 917 waliotahiniwa 1,638 walifaulu kwa daraja la 1-4 sawa na asilimia 92 ukilinganisha na mwaka 2015 walipotanihiniwa wanafunzi 2,386 na wanafunzi 858 kufaulu iliyokuwa asilimia 40.

•Kuwezesha upatikanaji vitabu vya kiada kwa wanafunzi wa Msingi na Sekondari. Tunaishukuru serikali kwa kupitia Taasisi ya Elimu kwa kutupatia vitabu 95,819 kwa Elimu ya Msingi, vitabu vya sanaa 10,603 vyenye thamani ya Tshs 84,824,000 kwa Elimu Sekondari kidato cha 1-4 na vitabu vya sayansi 3,251 vyenye thamani ya Tshs. 32,510,000 kwa kidato cha 5-6.

•Kufanya msambazo wa walimu wa Shule za Msingi kwenda kwenye Shule zilizokuwa na walimu wachache kupitia fedha za P4R.

•Kuboresha miundombinu katika baadhi ya Shule za Msingi na Sekondari kwa kupitia fedha za ufadhili wa P4R, Mapato ya Ndani, CDG ,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Waheshimiwa Wabunge, Mfuko wa Jimbo na wafadhili binafsi. Miundombinu hii ni pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo, tenki la maji, ukarabati wa maabara, kukamilisha madarasa yaliyokwama ujenzi kwa muda mrefu, ujenzi wa mabweni, kukarabati nyumba za walimu na kuanza ujenzi wa nyumba mpya za walimu na kutekeleza agizo la Mheshimiwa Rais la utengenezaji wa madawati.

•Kuanzishwa kwa Shule mpya ya kidato cha 5 Kikaro kwa tahasusi ya CBG. Shule hii tayari imeshapata usajili na ina wanafunzi.  

•Kuanzishwa kwa Shule za Msingi 8,  Kwamkomba, Kwamakuru, Changa, Tobola, Mbukwa, Visakazi, Komkwazu na Komtonga ambazo zinajengwa kwa nguvu za wananchi, mapato ya ndani ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa Elimu. Panapo majaaliwa tunatarajia mwaka 2018 zipate usaji wa kudumu na kuanza kupokea wanafunzi wa awali na Msingi.


Pamoja na mafanikio hayo zipo changamoto mbalimbali zinazotukabili katika uendeshaji na utoaji wa huduma ya Elimu Msingi. Changamoto hizi ni kama ifuatavyo:-

•Ukosefu wa gari kwa Idara za Elimu ya Msingi na Sekondari kwa ajili ya ufuatiliaji

•Ukosefu wa vitendea kazi vya shughuli za kila siku ofisini

•Upungufu mkubwa wa walimu kwa Shule za Msingi na kwa Elimu Sekondari kwa masomo ya sayansi. Awali idara ya Elimu Msingi ilikuwa na upungufu wa walimu 466. Kwa sasa ina upungufu wa walimu 496. Ongezekeo hili limetokana na walimu 30 kukumbwa na sakata la vyeti feki. Kwa upande wa Elimu Sekondari kuna upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi 71.

•Kutoletewa fedha za chakula cha wanafunzi kwa Shule ya Sekondari Kikaro pamoja na juhudi zilizofanyika.

•Miundombinu chakavu hasa kwa Shule za Msingi na Shule kongwe za Sekondari.

•Upungufu mkubwa wa nyumba za walimu.

•Uhitaji wa Shule mpya ya Sekondari Kata ya Pera na upanuzi wa Shule ya Sekondari Mdaula  ili kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika Shule ya Sekondari Chalinze.

•Majanga ya mara kwa mara yanayozikumba Shule zetu ambayo huharibu miundombinu ya Shule.  Kwa mwaka 2017 Shule 5 zilikumbwa na majanga ya kuezuliwa vyumba vya madarasa 10 na 2 (viwili) kubomoka kabisa, nyumba za walimu 2 zimeezuliwa na 2 kubomoka kabisa. Kuharibika kwa vifaa vya wanafunzi wanaosoma Chalinze Mzee baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko.

Aidha Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mh: Said Zikatimu ambaye ni mwenyekiti wa Halmahauri ya Chalinze amewataka Walimu na watendaji wote kufanya kazi kwa ueledi na kujituma ili kuleta maendeleo ya kitaaruma katika Halimashauri ya Chalinze. Pia aliwataka wanafunzi kuwa wasikivu na watii wawapo darasani kwani ni njia pekee itakayo sababisha wao kuweza kufanikiwa katika masomo na maisha yao kwa ujumla
Akizungumza mbele ya umatati wa watu Mh.Saidi Zikatimu amewaponge wanafunzi wote walioshiriki katika maonesho ya kitaaruma yalioandaliwa kwa ajili ya siku hiyo na kutoa mapendekezo kwa miaka mingine maadhimisho hayo yafanyike siku zisizopungua mbili ili sikumoja iwe ya maaonesho ya kitaaruma ili kuwapa wanafunzi wengi zaidi fulsa ya kushiriki katika maonesho hayo kwani kwa kufanya hivyo watajengewa uwezo mkubwa zaidi wa kufahamu mambo mbalimbali ya kitaaruma na mwisho wa siku kuweza kufauru vizuri zaidi katika mitihani yao ya mwisho

Mwisho mgeni rasimi aliwashukuru na kuwapongeza wanafunzi wote waliopata zawadi za kitaaruma kwa kufanya vizuri katika masomo yao pamoja na walimu wao, pia alito wito kwa watendaj wote katika sekta ya elimu ''JUMA LA ELIMU LIWE CHACHU NA KICHOCHEO CHA MAENDELEO YA TAARUMA KWA HALMASHAURI YA CHALINZE''








Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.