• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kaimu Mkurugenzi TAMISEMI Afungua mafunzo ya wakuu wa Idara na Vitengo Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere

Imewekwa: October 13th, 2025



Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bi. Lemi Shumbusho, leo amefungua rasmi mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze. Mafunzo hayo yanafanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bi. Shumbusho aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze kwa hatua ya kuandaa mafunzo hayo muhimu kwa viongozi wake. Alisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya dhati ya uongozi wa halmashauri katika kuhakikisha watumishi wake wanakuwa na ujuzi na maarifa ya kiuongozi yanayolenga kuongeza tija na ufanisi katika utendaji kazi wa kila siku.


Aidha, Bi. Shumbusho alisisitiza kuwa uongozi wa halmashauri una jukumu kubwa la kuhakikisha mafunzo haya yanakuwa chachu ya mabadiliko chanya katika utoaji wa huduma kwa wananchi. Aliongeza kuwa viongozi waliopewa dhamana wanapaswa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za nchi ili kuepuka changamoto zinazoweza kuathiri utekelezaji wa majukumu yao ya kitaifa.


Katika hotuba yake, Kaimu Mkurugenzi huyo alitoa pongezi maalum kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bw. Ramadhani Possi, kwa ubunifu na maono ya kupanga na kutekeleza mpango wa mafunzo haya. Alisema hatua hiyo ni mfano wa kuigwa na halmashauri nyingine nchini ambazo zinapaswa kuwekeza katika mafunzo ya watumishi wake ili kuongeza ufanisi wa taasisi zao.


Bi. Shumbusho aliwataka Wakuu wa Idara na Vitengo kutumia vyema fursa waliyoipata kwa kujifunza, kubadilishana uzoefu, na kuimarisha uwezo wao wa kiuongozi. Alisisitiza kuwa maarifa yatakayopatikana kupitia mafunzo hayo yanapaswa kutafsiriwa katika matokeo chanya kwa wananchi wa Chalinze na taifa kwa ujumla.


Mafunzo hayo yanatarajiwa kudumu kwa siku kadhaa yakihusisha masuala ya uongozi, usimamizi wa rasilimali watu, mipango na bajeti, pamoja na uwajibikaji katika sekta ya umma. Kupitia mafunzo hayo, Halmashauri ya Chalinze inalenga kujenga timu imara yenye uwezo wa kusimamia maendeleo endelevu na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kaimu Mkurugenzi TAMISEMI Afungua mafunzo ya wakuu wa Idara na Vitengo Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere

    October 13, 2025
  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze afungua mafunzo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu

    September 26, 2025
  • Maadhimisho ya wiki ya elimu ya watu wazima yafanyika Chalinze

    September 03, 2025
  • Tume ya Utumishi wa Umma Kufanya Ukaguzi Chalinze

    September 01, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.