• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kamati ya Afya ya Msingi yaweka Mikakati ya Mapambano dhidi ya Polio

Imewekwa: April 28th, 2022

Kamati ya afya ya msingi ya halmashauri ya chalinze imefanya kikao juu ya kampeni ya Chanjo ya Polio kwa watoto chini ya miaka mitano ambapo kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo Bi.Kasilida Mgeni kwaniaba ya Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo.

Katika hotuba ya Mwenyekiti wa kikao hicho Bi. Kasilida Mgeni aliwaelezea washiriki wa kikao kuwa lengo la Chanjo hiyo ya Polio ni kuweza kuchukua tahadhari za haraka na kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini kwani tayari Serikali ya Malawi mnamo tarehe 17 Februari, 2022  ilitoa tamko la kuwepo kwa mlipuko wa ugonjwa huo wa polio, hivyo basi ni kawaida wizara ya Afya kufuatilia kwa ukaribu taarifa za magonjwa ya mlipuko yanayozuilika katika nchi jirani kama vile Surua, Rubella na Polio ili kuweza kuchukua tahadhari za haraka na kuzuia magonjwa hayo yasiingie nchini kutokana na mwingiliano wa watu katika shughuli za kibiashara au kijamii.

Aidha Bi.Kasilida Mgeni aliwataka Washiriki na wajumbe wa kikao hicho kujipanga na kuwa  mabalozi wazuri kuhusu zoezi la chanjo ya polio kwa watoto chini ya miaka mitano na kutoa onyo kwa wote wanaopotosha zoezi hilo la chanjo kuacha mara moja.

“Niwaombe washiriki wote katika kikao hiki tutoke na mikakati madhubuti itakayolenga kuwafikia Watoto wote chini ya miaka mitano kupata chanjo na kufikia malengo zaidi na mkawe mabalozi wazuri kwenye jamii zenu na makundi yenu ili zoezi hili la chanjo ya polio liweze kufahamika na kueleweka vizuri kwa wananchi na niwaombe wakati wa uratibu wa zoezi hili kuangalia makundi maalumu nao waweze kupata haki yao ya msingi pia nitoe onyo kwa wote wanaopotosha juu ya zoezi hili kuacha mara moja kwani hakuna manufaa yoyote wanapofanya hivyo” Alisema Bi. Kasilida.

Nae mganga mkuu wa Wilaya Dkt.Allen Mlekwa alielezea ni kwa namna gani ugonjwa wa polio unaweza kuambukiwa pamoja na maadhara ya ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa Polio unasababishwa na kirusi cha Polio ambacho huambukizwa kutoka kwa mtu alieathirika kwenda kwa mwingine kwa kunywa au kula chakula au kinywaji kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya ugonjwa wa Polio na Virusi hivyo huzaliana katika utumbo na huweza kuathiri mfumo wa fahamu ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa viungo ndani ya masaa machache hata kupelekea kifo na ugonjwa huu huathiri zaidi Watoto chini ya miaka kumi na mitano na ugonjwa huu hauna tiba, njia kuu ya kuzuia ugonjwa huu ni kwa kuwapatia Watoto chanjo ya Polio iliyotengenezwa maalum kukinga ugonjwa huu ” Alisema Dkt.Mlekwa.

Kwa upande wa mratibu wa zoezi hili Halmashauri ya Chalinze Bw.Aidano Mbulinyingi ametoa maelezo ni kwa namana gani zoezi hili la kampeni ya kutoa chanjo ya polio litafanyika katika ngazi ya Halmashauri

Kampeni hii imelenga kutoa huduma kwa jumla ya walengwa 42365 ambao ni watoto wa miezi 0-59 na itafanyika kwa utaratibu wa kutoa Chanjo Majumbani (nyumba kwa nyumba), kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kliniki tembezi kwenye maneo maalum (Stendi, Sokoni, Machimboni)”Alisema Bw.Mbulinyingi.

Kikao hicho cha kampeni ya Chanjo kimehudhuriwa na Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama,Katibu Tawala wilaya, Mganga Mkuu wa Wilaya, Wajumbe wa timu za uendeshaji wa huduma za Afya wa Wilaya,Viongozi wa Madhehebu ya Dini,Wawakilishi wa vyama vya kisiasa, na Wajumbe wote wa Kamati ya Afya ya Msingi ya Wilaya.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.