• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kamati ya Siasa yafurahishwa na utekelezaji wa miradi ya Maendeleo Chalinze

Imewekwa: September 18th, 2023


Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani  imeridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika Halmashauri ya wilaya ya Chalinze,Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Abdulsharrif Zahoro imefanya ukaguzi wa Miradi mbalimbali ya maendeleo leo hii katika sekta za afya ,elimu na maendeleo ya Jamii katika kata za Bwilingu,Msoga,Lugoba na Mbwewe.


Wakikagua miradi hiyo wajumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Bagamoyo waliweza kukagua ujenzi wa soko la kisasa la Bwilingu na kuweza kujionea ubora wa soko hilo kwa jinsi lilivyojengwa katika viwango vinavyotakiwa kwa kuzingatia thamani halisi ya mradi na fedha zilizotumika yaani” Value for Money.” Soko hilo limejengwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri.


Hali kadhalika kamati ya siasa ilitembelea shule ya msingi Chalinze na kuweza kukagua ujenzi wa Bweni la watoto wavulana wenye mahitaji maalum na uzio wa Bweni hilo,wajumbe wa kamati hiyo waliweza kutoa ushauri wao juu kukamilisha bweni hilo kwa kuweka vitanda ili liweze kutumiwa na wanafunzi, akijibu hoja hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze Bwana Ramadhani Possi aliihakikishia kamati kuwa halmashauri imetenga fedha kwa ajili ukamilishaji wa bweni hilo sanjari na kununua vitanda.


Kamati ya siasa iliweza kufika katika Hospitali ya wilaya ya Chalinze ijulikanayo kama Msoga na kuona ujenzi wa Kituo cha Dharura cha Matibabu kilichojengwa katika Hospitali ya Msoga na kinaendelea kufanya kazi na wananchi wanaendelea kunufaika na huduma hiyo. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Bagamoyo Mheshimiwa Zahoro aliishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi inavyotekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuboresha Huduma za Afya na kutoa huduma zenye viwango na kuimarisha afya za wananchi.


Kamati ya siasa ilifurahishwa na ujenzi wa shule mpya ya sekondari inayojengwa katika kata ya Mbwewe kwa fedha kutoka serikali kuu. Halmashauri ya Chalinze ilipokea jumla ya fedha za kitanzania Milioni 528 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na ujenzi unaendelea,kamati imewataka wasimamizi wa mradi kusimamia kwa weledi na uaminifu ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.


Hata hivyo kamati ya siasa wilaya ya Bagamoyo,pamoja na miradi hiyo imeupongeza uongozi wa Halmashauri ya Chalinze kwa maana ya Baraza la madiwani na Menejimenti ya Halmashauri kwa usimamizi bora wa miradi ya maendeleo sanjari na ubunifu wa miradi mingi inayotekelezwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri, kama mradi wa kufyatua matofali unaendelea kusimikwa katika kijiji cha Lugoba kata ya Lugoba. Mradi huo utatumika kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika halmashauri kwani miradi hiyo itakuwa na ubora kutokana na ubora wa tofali zitakazo zalishwa na kiwanda cha halmashauri.


Naye Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Mheshimiwa Halima Okash ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa wilaya aliipongeza Halmashauri ya wilaya ya Chalinze kwa utekelezaji bora wa miradi ya maendeleo katika sekta za Afya,Elimu na mingineyo na kumshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuijali halmadhauri ya Chalinze kuipatia fedha nyingi kwa misingi ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kutatua kero za wananchi kama ilivyo ahidiwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020-2025.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.