• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia yawafikia Wananchi wa Mkange

Imewekwa: February 27th, 2025



Kampeni ya Msaada wa Kisheria imewafikia wananchi wa Kata ya Mkange katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, ikiongozwa na Mratibu wa kampeni hiyo, Wakili Asia Festus kutoka Wizara ya Sheria na Katiba. Kampeni hiyo inalenga kutoa elimu ya sheria kwa wananchi na kuwawezesha kuelewa haki zao za kisheria katika masuala mbalimbali.


Kampeni hiyo ilianza kwa kutoa elimu ya sheria kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Mkange, ambapo walifundishwa mbinu mbalimbali za kupambana na ukatili wa kijinsia na haki zao za msingi kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009. Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo wa kujitambua na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyoweza kuwakumba.


Akitoa elimu hiyo kwa wanafunzi, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bi. Atuganile Chisunga, aliwaelimisha kuhusu namna ya kutambua na kuchukua hatua dhidi ya vitendo vya ukatili. Aliwasihi wanafunzi kutoa taarifa kwa walimu wao, maafisa ustawi wa jamii, maafisa watendaji wa vijiji au mitaa, au mtu yeyote wanayemwamini wanapokumbana na viashiria vya ukatili.


Kwa upande wake, Mwanasheria Bw. John Mlyambate alitoa elimu kwa wananchi wa Kijiji cha Mkange kuhusu sheria za mirathi na wosia. Aliwahimiza wananchi kuzingatia sheria hizo katika mgawanyo wa mali za marehemu ili kuepusha migogoro ya kifamilia na kijamii.


Wakili Philimon Mganga alieleza kwa kina kuhusu sheria za ndoa na mgawanyo wa mali za wanandoa pindi wanapotalikiana kwa mujibu wa sheria. Aliwataka wananchi wa Mkange kutumia msaada wa kisheria kutoka kwa wasaidizi wa sheria wanapokumbana na migogoro ya ndoa ili kuhakikisha haki zao zinalindwa.


Naye Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Bw. Bartazari Mmiti, alitoa elimu kuhusu umiliki wa ardhi na aina za ardhi kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Alisisitiza umuhimu wa wananchi kufuata taratibu za kisheria katika umiliki wa ardhi ili kuepusha migogoro ya ardhi katika jamii.


Wananchi wa Mkange walionesha shukrani kwa kampeni hiyo, wakisema kuwa imewapa uelewa mpana wa masuala muhimu ya kisheria yanayogusa maisha yao ya kila siku. Waliomba kampeni kama hizi ziendelee kufanyika mara kwa mara ili kuwafikia wananchi wengi zaidi, hususan walioko maeneo ya vijijini ambako elimu ya sheria ni adimu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Chalinze yapongezwa kwa Hati Safi Mfululizo miaka mitano

    June 18, 2025
  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.