• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Katibu Mkuu afanya kikao na Watumishi wa Halmashauri ya Chalinze

Imewekwa: November 16th, 2022

                               Na John Mlyambate 

Katibu Mkuu wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Profesa Riziki Shemdoe leo amefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze Ndugu Ramadhani Possi.


Amepokea taarifa ya Ujenzi wa madarasa ya wanafunzi watakaoanza masomo yao ya kidato cha kwanza mwaka 2023,Ujenzi wa madarasa hayo ni kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan jumla ya fedha za kitanzania Bilioni 1.2. Ambazo zinaendelea kutumika katika ujenzi wa jumla ya vyumba vya madarasa 60.


Katibu Mkuu amepokea taarifa ya Ujenzi wa miundombinu ya afya katika Hospitali ya Halmashauri ya Msoga na vituo vya afya vinavyoendelea kujengwa kutokana na fedha zinazoletwa na Serikali.


Katibu Mkuu baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji alifanya kikao na Watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete,katika kikao hicho Katibu Mkuu alizungumza na Watumishi na kuwapongeza  kwa utendaji kazi uliotukuka kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Maendeleo,ukusanyaji mapato na utoaji huduma kwa wananchi ambao ndiyo waajiri wakuu.


Profesa Shemdoe aliwapongeza watumishi wote wanaomsaidia katika kutekeleza Majukumu mbalimbali kwa niaba yake kuanzia Katibu Tawala wa Mkoa,Wakurugenzi wote wa Mkoa wa Pwani ,Wakuu wa Idara na Vitengo na Watumishi wote ndani ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa nafasi zao na kuwataka Watumishi kuwa na ushirikiano na upendo katika maeneo ya kazi kwani mahali pa kazi ni mahali ambapo Watumishi wanatumia muda mwingi katika maisha.

“ Nisingependa kuona Watumishi wanakuwa watu wakutafutiana makosa na kuharibiana kazi kwa majungu si kitu kizuri,tulipo hapa kama Watumishi tumebeba dhamana na mizigo ya watu wengi nyuma yetu wanaotegemea kuishi kutokana na ajira tulizonazo,hivyo nawasihi tupendane na kuelekezana pasipo kuumizana.” Katibu Mkuu alisema.


Katibu Mkuu alimalizia kwa kuwataka Watumishi wafanye kazi kama timu kwa kushirikiana na Madiwani kwani bila Menejimenti ya Halmashauri imara na Madiwani imara hakuna Halmashauri,hivyo aliitaka Menejimenti ya Halmashauri kufanya kazi yake kwa weledi ili Halmashauri iweze kusonga mbele na hatimaye kuweza kutenda haki kwa wananchi kwa kuwaletea huduma muhimu za kijamii kama Elimu,Afya,Maji na nishati ya umeme.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.