• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

KEDA yatoa vigae vyenye thamani ya Milioni 46 kukamilisha ujenzi shule za sekondari mbili Chalinze

Imewekwa: August 5th, 2023


                          Na John Mlyambate,Chalinze

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amepokea vigae vyenye thamani ya Fedha za kitanzania millioni 46 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule za Sekondari za Miono na Jakaya Mrisho Kikwete. Mheshimiwa Ridhiwani amepokea vigae hivyo leo hii kutoka kampuni ya uzalishaji vigae ya KEDA iliyopo katika kitongoji cha Pingo katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Chalinze.


Vigae hivyo vimetolewa na kampuni hiyo ya KEDA kama wadau wa maendeleo katika Halmashauri ya Chalinze hususan katika sekta ya Elimu ili kuboresha miundombinu mbalimbali ya kielimu ili kuinua kiwango cha ufaulu ndani ya halmashauri.


Akisoma taarifa ya mapokezi ya vigae hivyo Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Chalinze Bi Salama Ndyetabura alieleza bayana kuwa vigae vilivyotolewa na kampuni ya KEDA ni kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule za Sekondari za Miono na Jakaya Kikwete ambazo kimsingi miundombinu yake ikikamilika italeta tija katika tendo la ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi wa Halmashauri ya Chalinze na watanzania kwa ujumla,Bi Salama aliishukuru kampuni ya KEDA kwa kujali umuhimu wa elimu na kuziomba kampuni zingine pia kuiga mazuri yanayofanywa na kampuni ya KEDA.


Mgeni Rasmi katika hotuba yake ya mapokezi ya vigae hivyo aliishukuru kampuni ya KEDA kwa kuyafanya matendo ambayo ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa vitendo na kwa niaba ya Chama chake cha Mapinduzi na serikali kwa ujumla na kuyataka makampuni mengine ambayo yanafanya kazi na Halmashauri ya Chalinze kuiga kwa vitendo uzalendo unaofanywa na KEDA.


Naibu Waziri aliendelea kuwataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili kuweza kufaulu mitihani yao vizuri kwani mazingira ya kujifunzia ni rafiki kabisa na hakuna sababu wala visingizio vya kutofaulu katika masomo yao,kwani miundombinu ya maji na umeme itakamilika kwa wakati pasipo kuchelewa. Mheshimiwa Ridhiwani aliahidi kuboresha miundombinu katika shule ya Jakaya Kikwete kwa kujenga nyumba Tatu za walimu.

“Tutanenga nyumba tatu za walimu ili walimu wakae hapahapa kwa ufanisi zaidi.” Ridhiwani alisema.


Naye Diwani wa kata ya Bwilingu,Mheshimiwa Nassa Karama aliishukuru kampuni ya KEDA kwa kuwa mdau wa maendeleo na elimu kwa ujumla,pia alimshukuru Mheshimiwa mbunge kwa niaba ya wananchi wake kwa jitihada zake katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Bwilingu na Chalinze kwa ujumla na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano wa hali ya juu katika jitihada hizo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze Bwana Ramadhani Possi alimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyofanikisha masuala mbalimbali ya kimaendeleo hususan katika uboreshaji wa miundombinu ya kiafya na elimu na kuahidi kuendelea kushirikiana bega kwa bega na Mheshimiwa Naibu Waziri kama Mtendaji Mkuu wa Halmashauri ili kutekeleza malengo ya Chama na serikali.


Afisa Biashara wa Kampuni ya KEDA Bwana Marcus Ma kwa niaba ya kampuni yake alisema ametoa jumla ya maboksi 1750 ya vigae yenye jumla ya fedha za kitanzania milioni 46 kwa shule mbili za Sekondari ambazo ni Jakaya Kikwete na Miono ili kuboresha miundombinu ya shule hizo. Maboksi 550 yametolewa kwa shule ya Jakaya Kikwete na maboksi 1200 yametolewa kwa shule ya Sekondari ya Juu Miono. Marcus Ma aliahidi kuendelea kushirikiana na Halmashauri ya Chalinze katika utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi sanjari na kutoa huduma kwa wananchi.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze Atembelea maonyesho ya 49 ya Saba saba

    July 14, 2025
  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Kampeni ya Ugawaji vyandarua bila malipo yazinduliwa Chalinze

    July 10, 2025
  • Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

    July 09, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.