• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kikao cha Wadau wa Maendeleo Chalinze Chafanyika

Imewekwa: November 19th, 2020

Kikao cha wadau wa Maendeleo katika halmashauri ya Chalinze kimefanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri katika eneo la Vilanda.Kikao hicho kinafanyika kama sehemu ya maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka 2021/2022.


Kikao hicho kimejumuisha wadau mbalimbali wa Maendeleo katika Jamii kama wafanyabiashara wakubwa,wajasiriamali, viongozi wa dini, viongozi wa asasi zisizo za kiserikali na viongozi wa kisiasa.


Akifungua kikao hicho cha wadau Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,Bwana Shabani Millao amewataka wadau kuanzisha vitega uchumi ambavyo vitainua uchumi wa Halmashauri ya Chalinze,na kuwataka wananchi wa Chalinze kuweka mazingira ambayo yatakuza mzunguko wa fedha katika halmashauri yetu na hatimaye kukuza uchumi." Wadau wa Maendeleo Chalinze inakuwa wilaya muda si mrefu na kutakuwa na msongamano wa watu wengi,hivyo wekezeni kwa kujenga hoteli na nyumba za kulala wageni uhitaji ni mkubwa na fursa ni za kutosha." Millao alisema.


Baada ya ufunguzi wa kikao hicho, Kamati ya Uwekezaji ya Halmashauri iliwasilisha mapendekezo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali kama dira ya ufanisi katika halmashauri ya Chalinze, mapendekezo ya miradi hiyo ni pamoja na uwekaji wa taa za barabarani,Msata,Mdaula, Lugoba,Vigwaza, Chalinze na Kiwangwa,Ujenzi wa maegesho ya magari,Mradi wa upimaji viwanja, Ujenzi wa eneo la mapumziko (Recreation center), Ujenzi wa uwanja wa michezo, Ujenzi wa vibanda vya maduka, Ujenzi wa stendi ya Bwilingu na uanzishaji wa kituo cha Redio Chalinze.


Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara katika halmashauri ya Chalinze Bwana Lawrence Peter aliipongeza Kamati ya Uwekezaji kwa maono yenye tija kwa maslahi ya wananchi wa Chalinze nakuweka msisitizo kwa Halmashauri kuwa na Mpango kabambe (Master plan) ya Mji wa Chalinze na kuyapima maeneo yote ya Taasisi za serikali ili kuyalinda na uvamizi unaoweza kufanywa na watu wenye nia ovu.


Kwa Upande wake Diwani Mteule wa kata ya Pera, Mheshimiwa Jackson Mkango aliunga mkono juhudi za makusudi zinazofanywa na halmashauri ya Chalinze Katika kuwaletea Maendeleo wananchi na kutoa ushauri wa namna ya kuboresha miundombinu ya barabara katika Mamlaka ya Mji mdogo wa Chalinze,ili maeneo yote ndani ya Mji wa Chalinze na vitongoji vyake yaweze kufikika kwa urahisi.


Naye Mwalimu John Kirumbi,ambaye ni Mwalimu wa shule ya Msingi Chalinze aliipongeza Halmashauri kwa kazi nzuri inazofanya sanjari na ujenzi wa soko la Bwilingu,aliwata watu wa Mipango Miji wanapokuwa wanapima na kuandaa michoro ya mpango kabambe wazingatie kutenga maeneo kwa ajili ya maziko kwani Mji unakuwa na Idadi ya watu inaongezeka.


Aidha Wadau wa Maendeleo waliitaka Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuwa na mapato ya kutosha kutekeleza miradi pendekezwa yote iliwasilishwa na Kamati ya Uwekezaji ya Halmashauri.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.