• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kilio cha wananchi wa Kaloleni Chaigusa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa

Imewekwa: March 13th, 2021

Kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa ikiongonzwa na Mwenyekiti wake Mh. Hamfrey Polepole imefanya ziara leo tarehe 13.03.2021 kijiji cha Kaloleni kilichopo kata ya Ubena Halmashauri ya Chalinze ili kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo inazotekelevya na mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF)


Akitoa neno la utangulizi Mh. Ridhiwani Kikwete (Mbunge wa jimbo la chalinze) alisema "kama viongozi hatupendi kuwapeleka sehemu zisizokuwa na matatizo tunapenda kuwaleta katika maeneo yenye changamoto ili mtusaidie, kwani kama Halmashauri kuna mambo tuliotekeleza lakini kuma mengine hatujafanikiwa yawezekana kwa sababu ya uwezo wetu kwa hiyo kwa ujio wenu hapa tuna imani mtatusaidia na wananchi wa Kaloleni na Chalinze kwa ujumla watanufaika"


Ni ukweli kua kamati hii imefanyika daraja la Utekelezaji wa majukumu baina ya wananchi na serikali yao mnapokuja kama kamati tunapata nafasi ya kueleza wananchi wanahitaji nini ili myasimamie na kuwanufaisha wananchi wanyonge wakiwemo wa Kaloleni, natambua kua kama kamati mmekua mkizunguka huku na huko kujionea na kukagua mambo ambayo serikali ya awamu ya tano imefanya chini ya uongozi wa Raisi wetu Mpendwa Mh. Dk John Joseph Pombe Magufuli nasi kama Chalinze tukisema tuanze yaelezea kwa kweli ni Mengi sana hatuta yamaliza aliongeza Mh. Kikwete.


Akizungumzia kuhusu wanufaika wa TASAF katika kijiji cha kaloleni Mh.Kikwete alisema "katika kijiji hiki chenye wananchi wasiopungua 1200 wanaoshi katika kaya maskini wasipungua 502 wananchi zaidi ya 218 wamekuwa niwanufaika wa TASAF, pia kupitia miradi mbalimbali wananchi wa kaloleni walijengewa bwawa la maji mwaka 2001 na kukamilika 2007 ambalo lilisaidia wanakaloleni na vijiji vya jirani. Aidha changamoto inayoikumba bwawa hilo ni pampu ya kusukuma maji kwenda kwenye chujio imeharibika na chujio lenye halifanyi kazi kitu kinachosababisa wananchi kukosa maji ya kunywa kwani maji yalitengenezewa mfumo wa moja kwa moja kitu kinachoweza sababisha wananchi kuathirika pale ambapo watayatunia bila ya kupati tiba stahiki, ni imani yangu kuwa ujio wenu tutapata suluhisho la changamoto hizo,


Akijibu hoja za changamoto zilizoainishwa kwenye taarifa ya mradi wa Bwawa la maji Kaloleni iliowasilishwa na Mtendaji wa kijiji Cha kaloleni Mbele ya M/Kiti wa kamati Mh. Polepole. Naibu waziri Ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi na Utawala Bora Mh. Deogratius Ndejembi alisema "tumezichua changamoto zote na tutahakikisha tunazipatia ufumbuzi ili Mh. Mbunge ukirudi Kaloleni uje kifua mbele na wananchi wa kaloleni waendelee kuwa na imani na serikali ya na Chama chao ambacho kimeshika Dola. Aidha Mh. Ndejembi aliahidi kurudi tena kaloleni kabla ya tarehe 28.03.2021 ili kujione kama maelekezo yote ya kamati kwa serikali yamefanyiwa kazi kwa kuwa serikali ya awamu ya tano haifanyi kazi kwa maneno bali kwa vitendo.


Nae Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na serikali za mitaa Mh. Polepole aliwataka wananchi  wairuhusu kamati kwenda na kukagua mradi wa Bwawa la maji ili aje kutoa maelekezo kwa serikali kwa niaba ya wananchi wa Kaloleni.


Akito maelekezo kwa serikali Mh. Polepole alisema kuwa "baada ya kujionea wenyewe eneo la mradi yako mambo ambayo kamati inaiagiza serikali kufanya kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa kaloleni na Chalinze kwa ujumla.


1.Kamati itapitisha bajeti ya wizara ili waendelee kuleta fedha ikiwemo kwa wanufaika wa TASAF pamoja na  wananchi wa Kaloleni

2.Kupitia utaratibu wenu wa kujihifadhia fedha na kuanzisha vikundi vyakukopeshana kwa kuwa mmetambua kua hatutaishi miaka yote kwenye TASSAF hivyo Halmashauri ya Chalinze wapatieni mikopo kupitia asilimia 10 ya vijana na kina mama wanavikundi hawa na muwatumie kama shamba darasa kwa wengine kwa kuwaongezea mtaji.

3. Kufuatia ubovu wa mfumo wa maji katika bwawa la Kaloleni TASAF na watendaji wote wanaohusika walekebishe mfumo wa maji katika Bwawa hilo ili yachujwe na yatoke yakiwa meupe safi na salama kwa matumizi ya binadamu na wanufaika wote wa Kaloleni na vijiji vya jirani mnatakiwa kusimamia mradi na  kuutunza ili uwanufaishe kwa muda mrefu.

4. Kwa kua eneo hili pia wapo wakulima kwani tunaona kuna migomba na mazao mengine hivyo sehemu ya kunyweshea mifugo iwe tofauti na sehemu ambapo wakulima wamelima mazao yao ili kutotengeneza migogoro isio ya lazima


Nao wanufaika wa TASAF akiwemo ndugu Juma Adhumani Rashidi aliishukuru Serikali kwa kuwasaidia kama kaya maskini na alisema kuwa kwa kutumia fedha alizopata kupitia TASSAF ameboresha shamba lake la mananasi hivyo ni matumaini yake kuwa hata mara baada ya mradi anaweza kujikimu kimaisha kwa kuwa TASAF imempatia msingi wa maisha kupitia fedha alizopata.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.