• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Kuwacheza Watoto wa Kike ni Kikwazo kwa Maendeleo ya Elimu Chalinze

Imewekwa: September 19th, 2018


Kuwacheza watoto wa kike ni moja ya sababu inayopelekea kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi katika halmashauri ya wilaya ya Chalinze. Wazo hili limebainika katika kongamano la wadau wa maendeleo lililofanyika jana katika Shule ya Msingi ya Msoga  kata ya Msoga.


Kongamano hilo limeandaliwa na uongozi wa kata ya Msoga kwa misingi ya kubaini changamoto ambazo ni kikwazo kwa maendeleo ya wanamsoga na wanachalinze kwa ujumla,kwa kuchambua changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo katika sekta za Elimu,Utawala Bora,Kilimo na Mifugo.


Katika kongamano hilo washiriki walianza kwa kubainisha changamoto zinazosababisha ufaulu duni kwa Elimu ya msingi na Sekondari.Akichangia katika kongamano hilo Mzee Herman Magomi alisema" Katika suala la utoaji Elimu kwa watoto linahusisha makundi matatu kwa maana ya walimu,wazazi na serikali,kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha suala la kutoa Elimu bora kwa watoto wetu linawezekana na ufaulu utapanda vinginevyo kama kutakuwa na kutothaminiana na kukwepa kutekeleza majukumu ya kila kundi hakutakuwa na ufanisi."Hermani alisema.


Naye Mwalimu Faraja Makala wa shule ya Msingi Lunga, alisema katika suala la kuhakikisha tunakuwa na ufaulu kwa watoto wetu ni kuwa na nidhamu ya kutekeleza majukumu yetu kama walimu, kwa maana ya kuingia darasani na kufundisha na wazazi kusimamia nidhamu ya watoto wao na kuwa karibu nao katika kuwashauri na kuwaeleza umuhimu wa Elimu katika jamii,lakini pia serikali itekeleze majukumu yake kwa kuhakikisha uwepo wa walimu kulingana na ikama kwa Shule husika sanjari na kushughulikia maslahi ya walimu kwa wakati na motisha mbalimbali kwa mujibu wa miongozo ya serikali."Yakitekelezwa haya kwa wakati na kila mmoja akatekeleza majukumu yake ufaulu utapanda." Faraja alisema.


Bi Grace Msinge,alisisitiza kwa kusema mabadiliko ya mitaala kwa Shule zetu na utumiaji wa vitabu mbalimbali katika ufundishaji na kujifunza ni moja ya changamoto zinazosababisha ufaulu duni tofauti na miaka ya zamani ambapo vitabu vilivyotumika vilikuwa ni vya aina moja,hata sasa ili kuinua ufaulu hatuna budi kuishauri serikali kutumia vitabu vya aina moja na kuachana na mabadiliko ya mitaala yasiyokuwa na tija.


Kwa upande wake Diwani wa kata ya Msoga,Hassani Mwinyikondo alitoa maoni yake katika kongamano hilo kwa kuwataka wazazi kuachana na tamaduni potofu za kuwacheza watoto wa kike wanapofikia umri wa kuvunja ungo wangali bado wanasoma Elimu ya Msingi hivyo kuwaathiri kisaikolojia na kushindwa kuendelea na masomo."Mtoto anapochezwa kwa mujibu wa utamaduni wa kabila la wakwele anakuwa yupo tayari kwa kuolewa na kuandaliwa kama mwali anaye subiri kuolewa,ili watoto wa kike waweze kusoma sisi kama wadau wa Elimu hatuna budi kupeleka mapendekezo ya kutunga sheria ndogo itakayo piga marufuku mtoto anayesoma Shule ya Msingi asichezwe mpaka atakapomaliza kidato cha nne."Mwinyikondo alisema.


Katika mjadala huo Kaimu Afisa Elimu Msingi,Edwin Kayuwi alitoa mchango wake katika kongamano hilo kwa kuungana na maoni ya wadau kwa changamoto zilizowasilishwa na kuwataka wazazi wawe chachu ya mafanikio katika kuinua kiwango cha ufaulu kwa kushirikiana na walimu katika kuijenga nidhamu ya mwanafunzi kama walezi lakini pia kuachana na tamaduni ambazo zinakuwa kikwazo cha mtoto katika kujifunza na tamaduni hizo zifanyike baada ya mtoto kuwa amefikia umri wa kujitambua na kujua baya na jema."Nasisitiza walimu kufundisha kwa bidii kwa kufuata miongozo ya Taaluma ualimu na kama idara ya Elimu Msingi tutaendelea kufanya marekebisho ya ikama kwa kadiri tunavyopata Fedha za uhamishi.",Kayuwi alisema.


Naye Diwani wa viti maalum na Mwenyekiti wa kamati ya Elimu,Afya na Maji Bi.Rehema Mno kwa niaba ya mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze aliwashukuru washiriki wa kongamano kwa kuwa wabunifu na kuandaa kongamano la kujadili changamoto zinazowakabili katika kata yao na kutafuta suluhu ya changamoto hizo na kuahidi kuwaunga mkono katika mapendekezo yao ya utatuzi wa kero kwa kushirikiana na ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Chalinze na kuwataka wadau wa Elimu kuwa mabalozi katika mapambano dhidi ya tamaduni mbovu zinazoathiri utoaji wa Elimu katika halmashauri yetu na kuwataka madiwani katika kata zingine kuiga mfano wa kata ya Msoga.


Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze Bwana Saidi Mwakapugi akichangia katika kongamano hilo aliahidi kuyapokea yote yaliyojadiliwa na kuyafikisha kwa Mkurugenzi mtendaji kwa hatua zaidi kwa maslahi ya wanachalinze kwa ujumla.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.