• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa TanzaniaYafana Chalinze

Imewekwa: December 9th, 2022


Maadhimisho ya miaka 61 ya Tanzania yafanyika na kufana vema katika wilaya ya Bagamoyo,maadhimisho hayo yamefanyika kiwilaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na kuchagizwa na vikundi mbalimbali vya sanaa sanjari na uwasilishwaji wa taarifa mbalimbali za mafanikio yaliyofikiwa na Serikali ndani ya miaka 61 ya Uhuru.


Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Lugoba mbele ya mgeni rasmi,Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo,Bi. Kasilda Jeremiah Mgeni. Kulifanyika shughuli mbalimbali kama michezo ya mpira wa miguu,upandaji miti,usafi wa mazingira na kongamo lililohusisha wananchi wote katika upokeaji wa mafanikio yaliyofikiwa na Serikali katika kuwahudumia wananchi na wananchi walipata fursa ya kutoa maoni yao kwa mafanikio ya Serikali katika sekta mbalimbali.


Katika kongamano hilo wataalam katika sekta mbalimbali walipata fursa ya kutoa maada mbalimbali kisekta na jinsi mafanikio yalivyopatikana ndani ya miaka 61 ya uhuru,maada zilizowasilishwa ni Siasa na Utawala Bora,Ufanisi katika Huduma za Jamii(Afya,Maji,Elimu na Nishati,Hali ya Uchumi,Kilimo,Viwanda,Biashara na Miundombinu.


Aidha wananchi walipata fursa ya kutoa maoni mbalimbali kuhusiana na mafanikio yaliyofikiwa ndani ya miaka 61 sanjari na kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ambayo ni:”Amani na Umoja ni Nguzo ya Maendeleo yetu.”

“Serikali yetu imepiga hatua kubwa katika suala la Utawala bora,kwani mwanzo maelekezo yalitoka juu kushuka chini lakini kwa sasa wananchi tunaweza kutoa mahitaji yetu kutoka chini kwenda juu kutokana na vipaumbele vyetu na yakafanyiwa kazi hii ni hatua kubwa kiutawala ndani ya miaka 61 ya Uhuru wetu.” Shekh Nassoro alisema.


Kwa upande wake Mgeni Rasmi katika kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya,Bi. Kasilda Mgeni aliwapongeza watoa mada wote katika kongamano hilo kwa kuweza kuyabainisha mafanikio ya Serikali kwa kina kisekta ndani miaka 61 ya uhuru wa Taifa la Tanzania na kuwataka washiriki wote kuwa mabalozi katika kuyasema mafanikio hayo hadharani kwani ndiyo uhalisia uliopo.


“Ndugu washiriki niwapongeze wote kwa jinsi mlivyoweza kuyasema kwa kina mafanikio ya Serikali katika nyanja mbalimbali za maisha,pia niwapongeze viongozi wote waliowahi kuliongoza Taifa hili kuanzia muasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Mzee Ali Hassan Mwinyi,Hayati Benjamin William Mkapa,Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli na Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa juhudi mbalimbali walizozifanya na zinazoendelea kufanyika katika kuliletea matokeo chanya Taifa hili.” Mgeni Rasmi alisema.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.