• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Maafisa Ugani Wapewa Pikipiki Chalinze

Imewekwa: February 7th, 2020


MKURUGENZI wa Halmashauri ya Chalinze Amina Kiwanuka amesema, shughuli za ugani katika Halmashauri hiyo zimekuwa na changamoto ikiwemo ya namna ya kuwafikia Wakulima ambao wapo katika Vijiji na Vitongoji huku maeneo mengine yakiwa hayana Maofisa Ugani.


Kiwanuka alibainisha hayo jana, wakati wa makabidhiano ya pikipiki kwa Maafisa Ugani, kutoka katika  vijiji  10  vilivyopo pembezoni ya Halmashauri hiyo.


Alisema, kutokana na changamoto ya Wakulima kutotembelewa kwa wakati,   wamekuwa hawapati huduma yenye tija kwa kutembelewa mara chache na wataalamu, na hivyo kuwa na uzalishaji hafifu.


Hali hiyo imepelekea Halmashauri  kupitia idara ya kilimo, kujiwekea malengo hadi kufikia 2021/2022 iweze kununua pikipiki 50, kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya Maafisa Ugani waliopo katika Kata na Vijiji.


Mkurugenzi huyo alisema, katika bajeti ya mwaka 2019/2020, Halmashauri hiyo ilitenga kiasi cha shilingi milioni 25 ambazo zimenunua pikipiki 10 kwa ajili ya Maofisa Ugani  katika vijiji vya pembezoni na zimekabidhiwa.


Aidha katika bajeti ya 2020/2021 kiasi cha shilingi milion 32 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki kumi, na kwamba wanatarajia kutenga fedha nyingine Shilingi milion 35.1 kwa ajili ya pikipiki 13 katika mwaka wa fedha 2021/2022 ili kukamilisha idadi ya pikipiki 50.


"Pikipiki hizi zitawasaidia Maafisa Ugani kuwatembelea Wakulima kwa wakati na  kuwapa huduma ambazo zitawawezeaha kuongeza tija katika shughuli zao za kilimo, na pia wataweza kufika katika Vijiji ambavyo havina Maofisa Ugani" alisema Mkurugenzi.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Zikatimu alitoa wito kwa maafisa ugani waliopata pikipiki hizo, kuhakikisha  wanazitumia kwa malengo yaliyokusudiwa, na kuepuka kuzitumia kama za biashara kwa kubeba abiria na kufanyia shughuli binafsi.


Zikatimu alisema, wananchi bado wanalima kilimo cha mazoea kutokana na kukosa wataalamu wa kuwapa elimu, upatikanaji wa pikipiki hizo utasaidia kukuza uchumi kupitia kilimo kwa Wakulima kupata elimu na ushauri.


Mmoja wa maafisa Ugani Aloyce Jumanne wa Kijiji Cha Kimange, aliishukuru Halmashauri hiyo kwa kuwawezesha kuwapatia usafiri ambao utawarahisishia utendaji kazi wao.


Mbali ya pikipiki hizo kumi, Halmashauri hiyo pia imepokea magari mawili Kati ya matatu, waliyoyanunua kupitia fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.