• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Madiwani Chalinze waikataa taarifa ya Ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA

Imewekwa: February 24th, 2024

MADIWANI wa Halmashauri ya Chalinze Mkoa wa Pwani wamekataa kupokea taarifa ya ujenzi wa Chuo Cha Ufundi (VETA) kinachojengwa katika  Kijiji Cha Magome kata ya Pera.


Wamekataa taarifa hiyo kwa madai kwamba mradi huo unasuasua huku fedha nyingi zikiwa tayari zinetumika tofauti na ilivyo katika maeneo mengine ambayo yamenufaika na mradi kama huo.


Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana Mjini Chalinze Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hassan Mwinyikondo alitoa maelekezo kwa vyombo vinavyoshighulikq na rushwa kufuatilia maendeleo ya mradi huo.


"Tunaagiza taarifa ikaandaliwe upya  na iletwe kwenye kikao, kuna taarifa ya sh. 300 milioni zinetumika katika ujenzi wa Chuo hiki lakini hata jamvi halijafunikwa hadi sasa,"alisema Mwinyikondo.


Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Halima Okash akizungumzia suala hilo alisema ushirikiahwaji wa maendeleo ya ujenzi wa Chuo hicho umekuwa ni hafifu huku akieleza kwamba fedha nyingi zinetumika lakini mradi hauonekani.


"Mradi huu uko kwenye Halmashauri yetu na umekuwa ukisuasua fedha zinapokuja inatakiwa zifanye kazi kwa haraka, suala hili nimelipokea na hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya anayehusika pia inatakiwa aandae mazingira Madiwani wakakague mradi huu," alisema Okash.


Mdhibiti ubora wa Shule Halmashauri hiyo ambaye ni msimamizi wa mradi huo Davis Moye akizungumzia kuhusiana na kukataliwa kwa taarifa yake  alisema shughuli za awali za ujenzi zilianza Julai 2023 zikisimamiwa na Mhandisi elekezi Taasisi ya Teknolojia Dar es Salam (DIT).


Moye alisema  baadae kazi hiyo ulishindwa kuendelea kwa muda kutokana na kukosekana kwa majibu ya vipimo vya udongo kazi iliyofanywa na chuo Cha ardhi Dar es Salam hawakuweza kukabidhi ripoti mshauri elekezi DIT jambo lililochelewesha kuanza kwa kazi ya ujenzi.


Kwa mujibu wa msimamizi huyo Juni 29, 2023 walipokea sh. Million 228,942.380 awamu ya kwanza ya fedha za ujenzi na  Septemba 2023 walipokea sh. 7,562.759 Milion kwa ajili ya usimamizi pia Desemba 2023 walipokea kiasi kingine cha sh.95,751,863.01kutoka Wizara ya Elimuna Teknoloji kwa ajili ya hatua nyingine za ujenzi.


Mradi huo ambao ulikadiriwa kukamilika Februari mwaka huu kwasasa ujenzi wake umefikia asilimia 35.44 na hadi kukamilika unatarajia kutumia sh. 1.5 Billion.


Mwisho

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.