• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Madiwani wa Masasi wajifunza mbinu za Ukusanyaji Mapato Chalinze

Imewekwa: December 8th, 2024



Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara leo wamefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Pwani, kwa lengo la kujifunza mbinu za ukusanyaji wa mapato na vyanzo mbalimbali vya mapato vinavyosaidia kuinua uchumi wa halmashauri hiyo.


Ziara hiyo imejumuisha madiwani 49 pamoja na wataalam wa Halmashauri ya Masasi wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Bi. Beatrice Mwinuka. Katika kikao cha ukaribisho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze, Mheshimiwa Hassani Mwinyikondo, aliwakaribisha wageni na kuelezea historia na mafanikio ya Chalinze tangu kuanzishwa kwake mwaka 2016.


Kwa mujibu wa Mheshimiwa Mwinyikondo, Halmashauri ya Chalinze ilianza kwa kukusanya mapato ya shilingi bilioni 3.8 kwa mwaka wa fedha 2016/2017, na sasa inatarajia kufikia makusanyo ya shilingi bilioni 17.2 kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Alibainisha kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano kati ya madiwani na wataalam wa halmashauri, pamoja na uwekaji wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji mapato.


“Mafanikio haya ni matokeo ya kazi ya pamoja kati ya viongozi wa kisiasa na wataalam. Tunazingatia uwazi na uwajibikaji katika kila hatua ya ukusanyaji wa mapato,” alisema Mheshimiwa Mwinyikondo.


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mheshimiwa Ibrahim Chiputula, aliishukuru Halmashauri ya Chalinze kwa kuwapa fursa ya kujifunza. Alisema kuwa mafunzo hayo yatachangia kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya Masasi.


“Ziara hii imetufungua macho. Tunawashukuru sana kwa ushirikiano wenu na tutaenda kutumia mafunzo haya kuboresha halmashauri yetu,” alisema Mheshimiwa Chiputula.


Madiwani wa Masasi pia walipata fursa ya kutembelea baadhi ya vyanzo vya mapato vya Halmashauri ya Chalinze na kujifunza mifumo ya kiutendaji inayotumika kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa ufanisi.


Ziara hiyo imelenga kubadilishana uzoefu baina ya halmashauri hizo mbili ili kuimarisha utendaji wa serikali za mitaa nchini.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.