• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

Imewekwa: June 11th, 2025



Na John Mlyambate,Chalinze


Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani, kwa lengo la kujifunza mbinu mbalimbali za ukusanyaji wa mapato ya ndani na utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotokana na mapato hayo. Ziara hiyo ilifanyika hivi karibuni na ilijumuisha madiwani pamoja na wataalam kutoka Halmashauri ya Pangani.


Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, Mheshimiwa Akida Omari Bahorera, ambaye aliongozana na wajumbe wa kamati yake pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo. Katika ziara hiyo, walitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayosimamiwa na Halmashauri ya Chalinze kwa kutumia mapato ya ndani.


Miongoni mwa miradi waliyoitembelea ni pamoja na ujenzi wa vyumba 80 vya maduka katika stendi ya mabasi ya Halmashauri iliyopo katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Chalinze, pamoja na soko la Bwilingu. Miradi hii inatajwa kuwa mfano bora wa matumizi ya mapato ya ndani katika kuboresha huduma kwa wananchi na kuongeza vyanzo vya mapato kwa halmashauri.


Aidha, madiwani hao walitembelea vizuia vya kukusanyia mapato ya ndani vilivyopo maeneo ya Lugoba na Kinzagu. Katika maeneo hayo walipata fursa ya kujifunza kwa kina mfumo wa ukusanyaji wa mapato, ikiwemo matumizi ya teknolojia na usimamizi wa vyanzo vya mapato ili kuhakikisha halmashauri inajitegemea kifedha.


Baada ya ziara hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani, Mheshimiwa Bahorera, alitoa pongezi kwa Halmashauri ya Chalinze kwa ubunifu na ufanisi katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya ndani. Alisisitiza kuwa Pangani imejifunza mambo mengi yenye manufaa ambayo wataenda kuyatekeleza katika halmashauri yao ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.


“Hakika tumejifunza mengi kutoka kwenu. Tunahakikisha mazuri haya tuliyoyaona tunayachukua na kuyatekeleza kwa manufaa ya wananchi wa Pangani na Watanzania kwa ujumla,” alisema Mheshimiwa Bahorera kwa niaba ya wenzake.


Ziara hii ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Pangani kujifunza na kuboresha mifumo yake ya ndani ya mapato pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo endelevu na kuboresha maisha yao kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mwenyekiti wa UWT akagua miradi ya maendeleo Chalinze

    June 13, 2025
  • Madiwani wa Pangani waipongeza Chalinze kwa Miradi ya mapato ya ndani

    June 11, 2025
  • DC Ndemanga Aongoza Kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe

    June 10, 2025
  • Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Tukamisasa waazimia Mwenyekiti Kupisha Uchunguzi

    June 10, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.