• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata yafunguliwa Rasmi

Imewekwa: August 4th, 2025


Na John Mlyambate 

Chalinze, Tanzania – Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Chalinze, Bwana Jovin Bararata, leo tarehe 4 Agosti 2025, amezindua rasmi mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025. Mafunzo haya yanawahusisha wasimamizi wasaidizi 30 kutoka kata zote 15 za Jimbo la Chalinze.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Bwana Bararata alisema kuwa mafunzo haya yatafanyika kwa siku tatu mfululizo na yanalenga kuwaandaa wasimamizi wasaidizi kwa kuwajengea uelewa wa kina juu ya wajibu wao, ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, uadilifu na weledi wa hali ya juu.


Bwana Bararata alisisitiza kuwa kazi ya usimamizi wa uchaguzi ni jukumu nyeti linalohitaji uaminifu, uzingatiaji wa sheria, pamoja na kuheshimu kanuni na taratibu za uchaguzi. Alisema kuwa wasimamizi hao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kuonyesha uadilifu na kutenda kazi kwa misingi ya haki na usawa.


Aidha, alikumbusha kuwa uteuzi wa wasimamizi hao umefanywa kwa mujibu wa sheria, hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanazingatia Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na kanuni zote zinazosimamia uchaguzi. Alieleza kuwa kutokuwa na uelewa wa sheria hizo kunaweza kusababisha kasoro zisizohitajika wakati wa uchaguzi.


Msimamizi huyo wa Jimbo aliwahimiza wasaidizi hao kuzingatia kila somo litakalotolewa katika kipindi chote cha mafunzo na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika mijadala na mazoezi ya vitendo ili kuongeza uelewa na kuondoa mashaka yoyote yanayoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.


Pia aliwakumbusha kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya kuhakikisha kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 unafanyika kwa amani, haki na kwa kufuata taratibu zote za kisheria, hivyo kila msimamizi msaidizi anapaswa kujitambua kuwa yeye ni sehemu muhimu ya mchakato huo wa kidemokrasia.


Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza ufanisi wa usimamizi wa uchaguzi katika ngazi ya kata na kusaidia katika kuhakikisha kuwa kila hatua ya uchaguzi inafanyika kwa uwazi, usahihi na kwa kuzingatia maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata yafunguliwa Rasmi

    August 04, 2025
  • Maandalizi ya Maonyesho ya Nanenane kanda ya Mashariki yapamba moto

    July 29, 2025
  • Halmashauri ya wilaya ya Chalinze kujenga kituo cha mafuta kwa mapato ya ndani

    July 16, 2025
  • Mkurugenzi Mtendaji Chalinze Atembelea maonyesho ya 49 ya Saba saba

    July 14, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.