• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mafunzo ya UWaWa yaanza rasmi Chalinze

Imewekwa: March 24th, 2023


,Mafunzo ya Kujenga Umoja baina ya Wazazi na Walimu wa Shule za Msingi na awali (UWaWa)  Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze yamefunguliwa rasmi hii leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe. Hassan Mwinyikondo katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Lugoba.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe.Hassan Mwinyikondo amelishukuru  Shirika la Shule bora kupitia mratibu wa Shule  bora Mkoa wa Pwani Bi. Oliva Kapaya kwa kuandaa mpango huo ambao utajenga umoja.

“Kwa dhati kabisa nilishukuru Shirika hili kupitia mratibu wake hapa Pwani kwani mpango huu unakwenda kujenga umoja baina ya wazazi na Walimu katika kusaidia suala la Elimu ndani ya Halmashauri na Taifa kwa ujumla na hili ni kuunga jitihada za Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika suala la Elimu nchini.”Alisema. Mhe Mwinyikondo

Hata hivyo Mhe. Mwinyikondo pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii,Afya na Maji Mhe. Selestine Semiono  wamewataka Wenyeviti wote wa kamati za Shule kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mafunzo yote wanayopatiwa yanakwenda kuufanyiwa kazai na kuwasilishwa  kwa wazazi wote ili waweze kuwa tayari kuendana na mpango huu wa Shule bora ili tuweze kuinua hali ya ufaulu katika shule zetu zote za chalinze na hatimaye kufikia daraja la juu la ufaulu.

Aidha Mhe.Mwinyikondo amesema kuwa wao kama Halmashauri watahakikisha kwa hali na mali wanaendelea kuunga mkono jitihada za shule bora kwa kuweka mpango wa ununuzi wa gari la kuchimba visima vya maji ili iweze kuchimba visima katika kila shule ili kuhakikisha upatikanaji wa maji ili watoto waendelee kula shuleni pamoja na kutoa zawadi kwa walimu na shule ambazo zitafanya vizuri katika matokeo ikiwa kama motisha.

Nae Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi. Mwl.Miriam Kihiyo amesema kuwa Mafuzo hayo yatadumu kwa siku 6 na yataweza kuwafikia Walimu wakuu wa Shule za Msingi pamoja na Wenyeviti wa  kamati za Shule zote  wakiwawakilisha wazazi wote wa Halmashauri ya Chalinze kwa lengo la kujenga umoja baina yao.

Kwa upande wa Mratibu wa Shule Bora na mafunzo hayo kwa Mkoa wa Pwani Bi. Oliver Kapaya ameeleza kuwa amefurahishwa na ujio wa Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Msoga kwani imeweka chachu katika kufanikisha suala zima la umoja wa Walimu na Wazazi lakini pia kwa jinsi Halmashauri inavyojipanga katika kuhakikisha mpango huo wa kuinua elimu unafanikiwa kwa asilimia mia na kuongeza ufaulu.

Kwaniaba ya Washiriki wa Mafunzo hayo ,Mwenyekiti wa kamati ya shule Shule ya Msingi Mbwewe Ndg. Iddi Aweso amesema kuwa mara nyingi wenyeviti wa kamati a shule huwa ndio vikwazo vikubwa lakini amewahakikishia viongozi hao kuwa watakwenda  kuyafanyia kazi yale yote waliyoyapata ili kuweza kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Elimu ndani ya Halmashauri ya Chalinze..

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.