• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mafunzo ya waandikishaji Daftari la kudumu la mpiga kura yafunguliwa Chalinze

Imewekwa: February 10th, 2025

Na John Mlyambate

 Afisa Mwandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wa Jimbo la Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, leo amefungua rasmi mafunzo ya uandikishaji wa wapiga kura kwa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kituo na waendesha vifaa vya BVR. Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Shule ya Sekondari ya Lugoba, yakilenga kuwajengea uwezo watendaji wa zoezi la uandikishaji wa wapiga kura.


Mafunzo haya yatachukua siku mbili, kuanzia tarehe 10 hadi 11 Februari 2025, na yanahusisha maelekezo ya kina juu ya taratibu za uandikishaji, matumizi sahihi ya vifaa vya BVR, pamoja na usimamizi wa kanuni na sheria za uchaguzi. Baada ya mafunzo haya, zoezi la uandikishaji wa wapiga kura litaanza rasmi kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari 2025 katika mikoa ya Pwani na Tanga.


Akizungumza wakati wa ufunguzi, Bwana Possi amewataka washiriki wa mafunzo kuwa makini, wasikivu, na waadilifu katika kazi zao ili kuhakikisha uandikishaji unafanyika kwa weledi na kukamilika kwa wakati, kulingana na ratiba iliyotolewa na Tume Huru ya Uchaguzi ya Tanzania. Amesisitiza kuwa jukumu walilopewa ni la kitaifa, hivyo wanapaswa kulitekeleza kwa uwajibikaji mkubwa ili kudumisha haki za wapiga kura.


Aidha, amewakumbusha washiriki kuzingatia viapo vyao walivyokula kabla ya kuanza mafunzo haya. Amewasisitiza kuwa viapo hivyo ni kwa mujibu wa sheria za nchi, zinazomtaka kila mtu anayehusika na majukumu ya kitaifa kutekeleza kazi kwa mujibu wa sheria, taratibu, na kanuni zilizowekwa. Amesema kutii viapo hivyo kutasaidia kulinda uadilifu wa mchakato wa uchaguzi.


Mafunzo haya ni sehemu ya maandalizi muhimu kuelekea zoezi la uandikishaji wa wapiga kura, ambalo ni hatua muhimu katika kuhakikisha kila raia mwenye sifa anapata fursa ya kushiriki katika uchaguzi mkuu ujao. Serikali na wadau wa uchaguzi wanaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato huu wa kidemokrasia.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.