• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mafunzo ya waandikishaji Daftari la kudumu la wapiga kura yafungwa rasmi

Imewekwa: February 11th, 2025

Na John Mlyambate


Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Chalinze, Bwana Ramadhani Possi, leo amefunga rasmi mafunzo ya waandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, yaliyofanyika kwa siku mbili mfululizo. Mafunzo hayo yalilenga kuwaandaa waandikishaji hao kwa ajili ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, unaotarajiwa kuanza rasmi Februari 13 hadi 19, 2025, katika Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze.


Katika hotuba yake ya kufunga mafunzo hayo, Bwana Possi aliwapongeza washiriki kwa kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika mafunzo hayo. Aliwataka kutumia maarifa waliyopata kwa ufanisi ili kuhakikisha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura linafanyika kwa weledi na mafanikio makubwa. Aidha, aliwahimiza kuzingatia maelekezo waliyopatiwa ili kuhakikisha kila raia mwenye sifa anapata fursa ya kuandikishwa.


Bwana Possi alisisitiza umuhimu wa utunzaji wa vifaa vya kazi vitakavyotumika katika zoezi hilo, akibainisha kuwa vifaa hivyo ni nyenzo muhimu katika kuhakikisha uboreshaji wa daftari unafanyika kwa ufanisi. Pia aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu kwa kuhakikisha wanahakiki taarifa zao na kujiandikisha ili waweze kushiriki katika uchaguzi ujao kwa mujibu wa haki yao ya kikatiba.


Katika kuimarisha huduma kwa wananchi, Afisa Mwandikishaji huyo aliwataka waandikishaji wote kufanya kazi kwa uadilifu, uwazi, na kwa kuzingatia maadili ya kazi zao. Alisisitiza matumizi ya lugha yenye staha na heshima kwa wananchi, akisema kuwa ni muhimu kujenga mazingira rafiki ili wananchi waweze kushiriki kwa uhuru katika zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia nchini.


Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni hatua muhimu katika maandalizi ya uchaguzi, hivyo ushirikiano kati ya waandikishaji na wananchi unahitajika ili kufanikisha zoezi hilo. Bwana Possi alihitimisha kwa kutoa wito kwa viongozi wa jamii, mashirika yasiyo ya kiserikali, na vyombo vya habari kusaidia katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • TANGAZO LA KAZI June 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Walimu wapewa maelekezo ya kazi Chalinze

    July 10, 2025
  • Kampeni ya Ugawaji vyandarua bila malipo yazinduliwa Chalinze

    July 10, 2025
  • Waziri Dkt Kijaji Azindua Kampeni ya Chanjo ya Mifugo Kitaifa Mkoani Pwani

    July 09, 2025
  • Waziri Kikwete Apokea Hundi ya Tsh Milioni 52 kutoka kiwanda cha Keda

    June 21, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.