• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mamlaka ya Bandari Tanzania Kujenga Gati Saadani

Imewekwa: July 13th, 2022

Mamlaka ya Bandari Tanzania imeamua kuirasimisha Bandari ndogo ya Saadani iliyopo katika Kijiji cha Saadani kata ya Mkange katika Halmshauri ya Chalinze kwa kujenga Gati itakayoipa uwezo bandari hiyo kutia nanga meli za mizigo na abiria,uamuzi huo umefikiwa leo katika kikao kilichofanyika katika kijiji hicho kati ya Uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania ,Mamlaka ya Hifadhi ya wanyama pori ya Saadani, Uongozi wa Halmashauri ya Chalinze na wafanyabiashara katika kijiji cha Saadani.


Akizungumza katika kikao hicho Afisa Mkuu wa Operesheni, Bwana Colman Moshi kwa niaba ya Mamlaka ya Bandari Tanzania aliwahakikishia washiriki wa kikao hicho kwamba ujenzi wa Gati hiyo utaanza mara moja baada ya kuwa utafiti umefanyika na kubaini ipi ni sehemu sahihi kwa kujenga Gati hiyo,na aliongezea kwa kusema utafiti huo kwa mujibu wa mtaalamu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania utafanyika ndani ya siku kumi na nne (14) ,baada ya hapo ripoti itawasilishwa kwa Mamlaka na utekelezaji unaanza maramoja.


Utekelezaji wa mradi huu wa Gati ni maombi ya Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete(MB) na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Miundombinu ili kuboresha biashara ya utalii katika Hifadhi ya Saadani na kuongeza mapato ya serikali na kukuza uchumi wa Saadani na wanachalinze kwa ujumla ,kwani baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Gati la Saadani itarahisisha ufikaji wa watalii kwa urahisi kutoka Zanzibar moja kwa moja hadi Saadani bila kupita Dar es salaam na kwa muda mfupi,kwani umbali kutoka Zanzibar hadi Saadani ni umbali wa kilomita 45.


Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Chalinze,Bwana Ramadhani Possi kwa niaba ya Menejimenti ya Halmashauri aliushukuru Uongozi wa Mamlaka ya Bandari kwa kukubali ombi la Mheshimiwa Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha ujenzi huu unakamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wananchi lakini pia kuvutia utalii katika halmashauri ya Chalinze na kuongeza mapato ya serikali kuu na Halmashauri.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.