• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mapato ya ndani kuimarisha huduma za maji vijijini

Imewekwa: March 30th, 2018

Halmashauri ya wilaya ya Chalinze imeamua kumaliza kero ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Magulumatali kata ya Talawanda kwa kuchimba bwawa la maji lenye uwezo wa kuhudumia wananchi zaidi ya 12,000,Mradi huu unatekelezwa kwa kutumia mapato ya ndani ya halmashauri, kama lilivyo agizo la serikali la kupeleka asilimia 60 ya mapato ya ndani yafanye kazi ya kuimarisha miundo mbinu ya maendeleo katika ngazi za vijiji na kata.

Kwa mujibu wa Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Mhe:Saidi Zikatimu alieleza kuwa utekelezaji wa mradi huu ni mipango mizuri ya halmashauri katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuhusu utoaji wa huduma mbalimbali za jamii kama upatikanaji wa maji vijijini,na kueleza thamani ya mradi huo ni zaidi ya milioni 29.

Aliishukuru Halmashauri yake kwa kuwa na mipango inayotekelezeka kwa wakati na kuondoa kero kwa wananchi na kuwashukuru watendaji wa halmashauri kwa kutekeleza mipango kwa vitendo kama inavyokuwa imepangwa katika vikao mbalimbali vya maamuzi.

Aidha Zikatimu alifafanua kuhusu ujenzi wa bwawa hilo kuwa lilijengwa mwaka 1995 wakati huo Mbunge wa Jimbo la Chalinze akiwa Rais Mstaafu Mhe:Jakaya Mrisho Kikwete likiwa na uwezo wa kuhudumia watu wasiozidi 2000,wakati huo kijiji hiki cha Magulumatali kikiwa kitongoji ndani ya kijiji cha Talawanda.Hivyo kwa sasa bwawa hili haliwezi kukidhi mahitaji ya wananchi wa Magulumatali kwani idadi ya wakazi imeongezeka.

Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji Bwana Ramadhani Biga kwa niaba ya wananchi wa Magulumatali aliishukuru serikali kwa jitihada zake katika kutatua kero za wananchi na kuongezea kuwa ujenzi wa bwawa hili ni utekelezaji wa kipaumbele cha wananchi wake kwani walihitaji huduma hii kwa muda mrefu sana.”Naomba serikali itutatulie kero ya barabara ya kutoka Lugoba kuja Magulumatali ili kurahisisha namna ya kusafirisha mazao tunayolima”.Biga alisema.

Naye Bwana Ali Mavula mkazi wa kijiji cha Magulumatali alieleza yake ya moyoni kwa kuupongeza uongozi wa halmashauri kwa kuwajengea bwawa na kuiomba serikali ifungue zahanati ya kijiji ili ianze kutoa huduma kwani majengo yamekamilika.”Tunaomba serikali ituletee watumishi wa afya ili tuweze kupata huduma mahali hapa”Mavula alisema.

Ujenzi wa bwawa la maji katika kijiji cha Magulumatali ukiendelea ili kuondoa kero ya maji kwa wananchi


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.