• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

MATHEOSTECHS Yafunga Umeme wa Jua Shule ya Sekondari Jakaya Mrisho Kikwete Chalinze

Imewekwa: February 23rd, 2024


Kampuni binafsi ya MATHEOSTECHS inayojishughulisha na ufungaji wa Umeme wa jua,uwekaji wa tovuti na wauzaji wa Vifaa mbalimbali vya Kielektroniki leo hii imefunga Umeme unaotumia nguvu za jua katika Shule ya Sekondari ya Jakaya Mrisho Kikwete iliyoko katika Kitongoji cha Msolwa katika kata ya Bwilingu,Mamlaka ya Mji Mdogo wa Chalinze. Kampuni hiyo imetoa msaada huo wa kufunga Umeme huo ili kuondoa kero ya ukosefu wa Umeme katika shule hiyo mpya iliyojengwa hivi karibuni kwa fedha za Serikali kuu.


Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bwana Theobald Boniventure,ameamua kufunga Umeme huo katika Shule ya Jakaya Mrisho Kikwete ili kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan za kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Umeme ulifungwa katika Shule hiyo umegharimu zaidi ya fedha za kitanzania Milioni 16 ili kuwawezesha watoto wa kitanzania kusoma kwa bidii usiku na mchana ili kufikia malengo yanayotakiwa kwa mujibu wa sera ya Elimu nchini Tanzania 


Shughuli ya uzinduzi wa huduma hiyo imefanywa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete. Mheshimiwa Kikwete amezindua kwa kukata utepe kama ishara ya kurasimisha matumizi ya Umeme huo katika shule hiyo na kuishukuru Kampuni hiyo kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Halmashauri ya Chalinze.

“Binafsi niishukuru kampuni ya MATHEOSTECHS Kwa uzalendo Mkuu na upendo wa hali ya juu,kwa kutambua uhitaji wa shule hii na kutoa msaada stahiki ili kuwawezesha wanafunzi wa shule hii zaidi ya 200 kuweza kusoma muda wowote pasipo shaka.” Mheshimiwa Ridhiwani alisema.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chalinze Bwana Ramadhani Possi ameishukuru Kampuni ya MATHEOSTECHS kwa kazi waliyoifanya na kuahidi Ushirikiano mkubwa na Kampuni hiyo katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili Halmashauri ya Chalinze.


Mkuu Divisheni ya Sekondari wa Halmashauri ya Chalinze Bi Salama Ndyetabura ameipongeza Kampuni ya MATHEOSTECHS kwa kuweka mazingira chanya ya kufundishia na kujifunzia yanayowamotisha wanafunzi kufikia malengo takiwa katika Elimu. Ndyetabura aliendelea kwa kuwasihi wanafunzi kuitumia fursa ya Uwepo wa Umeme wa jua kujisomea kwa bidii na kufanya vema katika mtihani wa Taifa.


Kwa upande Wake Mkuu wa Shule ya Jakaya Mrisho Kikwete Mwalimu Benedikto Mwakilema akitoa taarifa ya Maendeleo ya Shule hiyo allishukuru Kampuni ya MATHEOSTECHS kwa huduma nzuri ya mwanga wa Umeme na kuiomba Serikali kukamilisha baadhi ya miundombinu ambayo haijakamilika shuleni hapo sanjari na ukamilishaji wa maabara za Sayansi,mabweni ya wanafunzi na nyumba za walimu.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.