• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mhe. Ridhiwani Kikwete apokea Vifaa tiba kutoka Taasisi ya LIONS CLUB

Imewekwa: September 30th, 2022

Mhe. Ridhiwani Kikwete apokea Vifaa tiba kutoka taasisi ya LIONS CLUB.

Naibu Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe.Ridhiwani Kikwete leo tarehe 29/09/2022 amepokea msaada wa vifaa tiba  kutoka taasisi ya LIONS CLUB INTERNATIONAL Mhe.Ridhiwani amevikabidhi  vifaa hivyo katika zahanati ya Ruvu darajani mbele ya Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze ili viweze kusaidia utoaji wa huduma za afya kwa wananchi na wakazi wa kata ya Vigwaza na vijiji jirani.

Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Mhe.Ridhiwani amewashukuru taasisi ya LIONS CLUB kwa msaada walioutoa na kwa kutekeleza Sera ya Mheshimwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha mahusiano.

“Kipekee kabisa nimefarijika sana kupokea vifaa hivi vya afya kutoka taasisi ya LIONS CLUB kwani mmekuwa wepesi sana kusikia kilio cha wana Ruvu darajani na hii ni kiashiria kwamba taasisi hii inatekeleza sera ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuimarisha mahusiano na muunganiko baina ya Serikali kuu na taasisi binafsi”.Amesema Mhe.Ridhiwani.

Hata hivyo Mheshimiwa Naibu Waziri ameendelea kuhimiza Halmashauri zote nchini ziweke utamaduni wa kutenga sehemu ya ardhi kwaajili ya miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi wa huduma za afya kwani ndio suala muhimu na la msingi kwa wananchi.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze Mhe.Hassan Rajabu Mwinyikondo amewashukuru wageni hao kwa msaada huo wa vifaa vya pamoja na kuwakaribisha kutumia fursa zilizopo chalinze hasa katika kununua ardhi iliyopo katika mipango miji katika mradi wa viwanja Msolwa.

“Niwashukuru sana taasisi hii kwa vifaa hivi mlivyotupatia na hata hivyo niwakaribishe sana Chalinze kwani kuna fursa nyingi za kuwekeza hivyo basi sisi kama Halmashauri tuna viwanja vingi na vyakutosha vya biabashara kwa bei nafuu”.Amesema Mhe.Mwinyikondo

Pamoja na hilo Mhe. Mwinyikondo amewaomba LIONS CLUB kuwa sehemu ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze 

Aidha  Mwenyekiti mstaafu wa LIONS CLUB  Ndg Muntadhir Baruan amesema kuwa si vifaa hivi tu vya afya vilivyotolewa siku ya leo bali watahakikisha wananchi wanapata huduma nyingine hususani kwenye sekta ya maji.

“Tulipokea maombi ya uhitaji wa vifaa vya huduma za afya katika Zahanati ya Ruvu Darajani na leo tunashukuru tumevikabidhi  lakini pia tunajua matatizo yako mengi hivyo basi sisi kama taasisi tutahakikisha tunaifikia jamii hasa katika masuala ya afya pamoja na maji”Amesema Ndg.Baruan.

Aidha Diwani wa kata ya vigwaza Mhe.Mussa Gama amezungumza kwaniaba ya wakazi na wananchi wa Ruvu darajani ambapo ametoa shukrani za dhati kwa taasisi ya LIONS CLUB kwa msaada huo kwani utasaidia utoaji wa huduma za afya katika kata hiyo.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa taasisi hii kwani msaada huu utapunguza changamoto za utoaji wa huduma za afya hasa kwa kina mama wajawazito katika zahanati yetu ya Ruvu darajani na ninaamini kupatikana kwa vifaa hivi huduma za kujifungua zitaendelea kuwa bora zaidi”.Amesea Mhe.Gama.

Vifaa tiba hivyo ni pamoja na vitanda 3, vitanda vya uchunguzi 2 ,magodoro 4 pamoja na hadubini 1 na hivi vyote vimegharimu kiasi cha shilingi milioni 5. 

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • PPRA yatoa Mafunzo ya NeST kwa Watendaji wa Kata na Wakuu wa Shule Chalinze

    May 08, 2025
  • Watendaji wa Kata na Vijiji wapewa Mafunzo ya namna ya kukusanya Kodi ya Majengo Chalinze

    May 07, 2025
  • PPRA yatoa mafunzo ya Ununuzi kwa watumishi wa Afya Chalinze

    May 07, 2025
  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango yafanya ziara kukagua miradi ya maendeleo

    May 06, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.