• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Mila na Dhana ya Ubaguzi wa Wanawake ni Tatizo katika Jamii

Imewekwa: September 25th, 2022


Sehemu kubwa ya mila na tamaduni za watanzania zimekuwa na mrengo wa kupendelea au kuegemea kwa wanaume zaidi na kubagua haki ya mwanamke katika kurithi au kumiliki mali. Ili kuweka usawa mbele ya sheria, mnamo mwaka 1999 Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ilifuta dhana nzima ya ubaguzi wa sheria za kimila. Kwa ufupi sheria hii ilileta usawa baina ya mwanaume na mwanamke katika kumiliki ardhi. Sheria imetamka kuwa;

“... sheria yoyote ya kimila inayowanyima wanawake, watoto au watu wenye ulemavu uhalali wa kumiliki mali, kutumia au kupata ardhi, basi sheria hiyo ya mila itakuwa batili...”

Pamoja na hayo, mila na desturi zimekuwa hazimtambuwi mjane kabisa katika dhana nzima kurithi mali za marehemu mume wake. Mila hazikuzingatia kabisa ushiriki au uchangiaji wa mjane katika kuchuma mali za familia ambazo mwisho wa siku hutambulika kama za mwanaume tu. Hata hivyo kwenye shauri la Maagwi Kimito vs Gibeno Werema Mahakama ya Rufani iliweka bayana kuwa sheria zote za kimila katika nchi hii lazima ziwe na hadhi sawa kwenye Mahakama kama sheria nyingine isipokuwa tu kama Katiba au sheria za nchi zitaelekeza tofauti. Kwa nukuu Mahakama ilisema: -

“...The customary laws of this country now have the same status in our courts as any other law subject only to the Constitution and any statutory law that may provide to the contrary...”


Kuna mifano kadhaa ambapo Mahakama zetu za juu zimetoa miongozo juu ya sheria za mila katika mirathi. Kwenye kesi ya Violet Ishengoma Kahangwa & Jovin Mutabuzi vs Administrator General & Mrs Eudokia Kahangwa Mahakama ya Rufani pamoja na mambo mengine ilielekeza kuwa;

“...that under paragraph 43 of the Local Customary Law (Declaration) (No.4) Order, 1963, G.N. No.436 as applied to the Bahaya tribe vide G.N. No. 605 of 1963, an illegitimate child cannot inherit from the father’s side upon his dying intestate...”

Kwa tafsiri rahisi Mahakama ya Rufani imesema kuwa katika mila za Wahaya mtoto wa nje hawezi kurithi mali za marehemu baba yake pale anapofariki bila ya kuacha wosia.

Mfano mwingine tunaupata kwenye shauri la Masudi Ally vs Chiku Masudi ambapo Mahakama Kuu ilisema:

“...that under paragraph 26 of the 2nd schedule of the Customary Law Declaration 436/1963 only children of the deceased have the right to inherit from their deceased’s parents’ property... it is the children - them alone - of the Deceased that are customarily entitled to inherit the entire property, (without exception), of their late father. The appellant having been a complete stranger to the family of the Respondent’s late father, he is equally a stranger to the property of the Respondent’s late father...”

Kwa Kiswahili Mahakama Kuu imesema kuwa ni watoto wa marehemu pekee wanaoweza kurithi mali za marehemu baba yao. Mtu baki haruhusiwi kurithi chini ya sheria za mila.

Inatupasa kuelewa vema kuwa kwenye shauri la Violet Ishengoma

(Supra) Mahakama ya Rufani ilitafsiri haki ya kurithi kwa mtoto wa nje ya ndoa kwa kuzingatia sheria za mila pekee. Hata hivyo kwa kwa upande mwingine na kwa kuzingatia kuzingatia Sheria ya Mtoto na shauri la Elizabeth Mohamed vs Adolf John Magesa Mahakama Kuu imesema kuwa mtoto wa nje ya ndoa anayo haki ya kurithi mali za marehemu baba yake. Pia kwenye shauri la Judith Patrick Kyamba vs Tunsume Mwimbe & 3 Others. ambapo pamoja na mambo mengine Mahakama Kuu imekuwa na mtazamo kuwa mtoto hapotezi haki ya kurithi mali ya mzazi wake kwa kigezo cha kuzaliwa nje ya ndoa. Kwa kuzingatia maamuzi ya Mahakama ya Kuu hadi sasa, (kwa kuwa bado maamuzi haya hayajatenguliwa na Mahakama ya Rufani) mtoto anastahili kurithi hata kama amezaliwa nje ya ndoa. Maamuzi haya ya Mahakama Kuu hayakinzani na maamuzi ya Mahakama ya Rufani kwenye shauri la Violet Ishengoma kwa kuwa sheria zilizotumika ni tofauti.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.