• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
    • Maoni |
Chalinze  District Council
Chalinze  District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halimashauri
    • Idara
      • Divisheni ya Miundombinu,Maendeleo ya Vijijini na Mijini
      • Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi
      • Divisheni ya Elimu ya Sekondari
      • Divisheni ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka ngumu
      • Kitengo cha Maliasili na Hifadhi ya Mazingira
      • Kitengo Cha Fedha na Uhasibu
      • Divisheni ya Mipango na Uratibu
      • Divisheni ya Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Divisheni ya Maendeleo ya Jamii
      • Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu
      • Divisheni ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
      • Kitengo cha Michezo,Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Huduma za Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Utaalamu
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha,Utawala na Mipango
      • Afya,Elimu na Maji
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Maadili
      • VVU/UKIMWI
    • Ratiba ya Vikao
    • Shughuli za Maendeleo za Madiwani
      • Kata ya Bwilingu
      • Kata ya Kibindu
      • Kata ya Kimange
      • Kata Kiwangwa
      • Kata ya Lugoba
      • Kata ya Mandera
      • Kata ya Mbwewe
      • Kata ya Mkange
      • Kata ya Msata
      • Kata Msoga
      • Kata ya Pera
      • Kata ya Tarawanda
      • Kata ya Ubenazomozi
      • Kata ya Vigwaza
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Service Client Charter
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Hatua
    • Miongozo
    • MATANGAZO
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video za shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha

Milioni 140 Kuneemesha Wanawake na Vijana Chalinze

Imewekwa: June 14th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze yatoa mikopo ya fedha za kitanzania milioni 140 kwa vikundi vya vijana na wanawake 39 vilivyokidhi vigezo kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri ambayo ni asilimia 10 ya mapato hayo.Zoezi la kukabidhi hundi kwa wajasiriamali hao limefanywa jana na Katibu Tawala wa wilaya ya Bagamoyo kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Bi Erica Yegela katika kijiji cha Msata.

Kwa mujibu wa Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya Bwana Saidi Mwakapugi,amesema mkopo huu kwa vikundi vya vijana na wanawake ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lakini pia ni mpango wa halmashauri kwa bajeti ya mwaka 2017/2018 ambayo halmashauri ilipanga kutoa mikopo kwa  wanawake na vijana jumla ya fedha za kitanzania milioni 300,mpaka sasa halmashauri imekwisha kopesha jumla ya fedha za kitanzania milioni 260.

Mwakapugi aliendelea kufafanua,kwa robo ya tatu halmashauri inatarajia kutoa mkopo wa  fedha za kitanzania milioni 169,hivyo kuvuka lengo kwa mwaka wa fedha 2017/2018.Utoaji mikopo kwa wanawake na vijana ni matokeo mazuri ya namna halmashauri inavyokusanya mapato na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hizo kwa mujibu wa bajeti na miongozo ya serikali.

Afisa Maendeleo ya Vijana Bi Wahda Mwishehe     katika taarifa yake kwa mgeni rasmi alisema,vikundi vya vijana na wanawake vinapopata mikopo hii hujishughulisha na shughuli mbalimbali za ujasiriamali kama utengenezaji wa mikeka,vikapu,machanuo,miko,mikoba ,shanga,utengenezaji wa sabuni na batiki na biashara ndogondogo, hivyo kurejesha mikopo kwa wakati na wadau wengine kukopeshwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Chalinze Mheshimiwa Said Zikatimu aliwaasa wanawake na vijana kujiunga katika vikundi ili kukidhi vigezo vya kuweza kukopesheka na kuwataka waitumie mikopo hiyo katika kujikwamua na umasikini wa kipato.Aidha Zikatimu alieleza mafanikio yaliyofanywa na halmashauri yake kuwa ni pamoja kuviwezesha vikundi vya wanawake na vijana kwa asilimia 100,kupeleka asilimia 60 ya mapato ya ndani katika miradi ya maendeleo katika sekta za Maji,Elimu,Afya,Barabara na Utawala.

Halmashauri kwa uwepo wake wa miaka miwili imeweza kununua magari matatu mapya kutokana na mapato ya ndani na kwa mwaka huu wa fedha tunatarajia kununua matrekta 6 katika kuboresha sekta ya kilimo hapa wilayani,lakini pia tumeweza kununua pikipiki 15 kwa ajili ya maafisa watendaji na maafisa ugani. Zikatimu alieleza.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Bi Erica Yegela katika hotuba yake aliishukuru halmashauri ya wilaya ya Chalinze kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi kwa kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia mipango na bajeti kwa mwaka husika.

Aidha Yegela aliwaasa wanawake na vijana kuitumia vizuri mikopo wanayopata kwa kuzalisha kwa tija na hatimaye kuondokana na umasikini wa kipato na akasisitiza waendelee kuwa waaminifu kwa kurejesha mikopo kwa wakati ili vikundi vingine pia viweze kupatiwa.

Katibu Tawala katika hotuba yake ya kukabidhi hundi kwa wajasiriamali hao aliwataka wananchi kwa ujumla kupambana na vitendo vya rushwa,kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI,na kutoa taarifa kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mara wanapoona kuna dalili ya uvunjifu wa amani katika maeneowanayoishi.

Wanawake na Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze wakisubiri kukabidhiwa hundi na Mgeni Rasmi,Katibu Tawala wa Wilaya,Bi Erica Yegela       




Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUBORESHA DAFTARI LA WAPIGA KURA February 03, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango chafanya kikao kujadili mapato na matumizi kwa mwezi Aprili 2025.

    May 31, 2025
  • Maafisa Habari watakiwa kuitangaza miradi ya serikali

    May 30, 2025
  • Halmashauri ya Chalinze yatembelewa na wawekezaji wa nyumba

    May 29, 2025
  • Kampeni ya "Ni rahisi sana"yatoa Elimu kuhushu usalama Mtandaoni Chalinze

    May 28, 2025
  • Tazama zote

Video

Ofisi ya Utumishi yakutana na Watumishi wa ajira mpya Chalinze
Video nyingine

Viungio vya haraka

  • Mfumo wa Kiuhasibu wa Kuripoti fedha katika Vituo (FFARS)
  • mfumo wa taarifa wa kiutumishi (ess)
  • RIPOTI YA MKAGUZI MKUU WA SERIKALI 2020/2021
  • Mfumo wa Vibali vya Kusafiri Nje ya Nchi
  • Mamlaka ya Serikali Mtandao
  • Jinsi ya Kusajili na kupata namba ya mlipakodi (TIN NAMBA)
  • mfumo wa mrejesho serikalini
  • mfumo wa manunuzi wa umma

Viungio vya tovuni mhimu

  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Tovuti ya Mkoa
  • Tovuti ya Serikali
  • Tovuti ya Utumishi
  • Baraza la Mitihani la taifa
  • Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira

Wasomaji Mbalimbali Dunia

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

Visitors Counter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    114 Morogoro Rd, 61383 Bwilingu

    Anuani ya posta: P O BOX 65 Chalinze

    Simu: +255232935403

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe : ded@chalinzedc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2018 chalinze district council . All rights reserved.